NA MWAMVUA MWINYI,BAGAMOYO

MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo amepiga marufuku uingizwaji wa mifugo katika eneo la kampuni ya Said Salim Bakhresa Group Ltd,ambalo amekusudia kuanza ujenzi wa kiwanda cha sukari Juni 2019 na uzalishaji ifikapo septemba 2020-2021. 

Aidha amewasihi wafugaji kuheshimu maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya uwekezaji na kilimo . Ndikilo aliyasema hayo ,wakati kamati ya siasa ya mkoani humo , ilipotembelea shamba hilo kujionea utekelezaji wa agizo la Rais alilolitoa kipindi cha nyuma baada ya kufungua kiwanda cha vinywaji baridi cha kampuni hiyo kilichopo Mkuranga.

Alisema agizo la Rais lilikusudia kuondoa pengo la uzalishaji wa sukari kwa matumizi ya kawaida nchini . Ndikilo, alisema mradi huo ni mkubwa na ni hazina kwa mkoa na kujivunia kupiga hatua ya kiuchumi na ujenzi wa viwanda.

Mkuu huyo wa mkoa alishauri sehemu ya mradi kuwe na wakulima wa nje ili kuwaondolea umasikini. Kuhusu fidia walioguswa na mradi huo alisema fidia inalipwa kwa awamu na taratibu za kuwafanyia tathmini hivyo ambao bado wavute subira lakini hawatolipwa wavamizi. Nae msimamizi wa mradi huo, Muharami Mkenge alielezea, kampuni ya Said Salim Bakhresa (SSB) Group LTD imekusudia kuanza ujenzi wa kiwanda Juni 2019 na uzalishaji wa sukari kiwandani ifikapo septemba 2020-2021. 
MKUU wa mkoa wa Pwani ,mhandisi Evarist Ndikilo akizungumza mbele ya Viongozi wa Serikali na Chama cha CCM,alipokuwa akitoa tamko la kupiga  marufuku uingizwaji wa mifugo katika eneo la kampuni ya Said Salim Bakhresa Group Ltd,ambalo amekusudia kuanza ujenzi wa kiwanda cha sukari Juni 2019 na uzalishaji ifikapo septemba 2020-2021.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...