NA RS TABORA.

MADIWANI wa Manispaa ya Tabora wameonywa kutojihusisha na biashara ya aina yoyote zinazotolewa na Ofisi ya Mkurugezi na wametakiwa kubaki kuwa wasimamizi wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

Onyo hilo limetoelwa leo na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa alipokuwa akizungumza na Madiwani,Watumishi wa Manispaa, watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na Watendaji wa ngazi mbali mbali wa taasisi za umma zilizopo Manispaa ya Tabora ikiwa ni siku ya tatu ya ziara yake mkoani humo.

Waziri Mkuu amewataka Madiwani ambao wanajihusisha na Kampuni zinazofanya biashara na Halmashauri ya Manispaa hiyo wajiondoe ili waweze kuchukua hatua pale inapotokea tatizo au dosari yoyote.

Alitoa wa mfano wa mradi wa ununuzi wa Magari mawili na kontena za kubebea taka ambao alipewa mmoja wa madiwani wa Manispaa hiyo ambaye hakumtaja jina. Waziri Mkuu alisema kuwa kampuni hiyo ilinunua magari hayo huku moja likiwa bovu na ili kuwadanganya zaidi alilipaka rangi ili lionokane ni jipya na hadi leo halijafanya kazi na hakuna hatua zilizochukuliwa kutokana na kulindana.

Aliongeza kuwa kampuni hiyo ambayo ilipewa kazi hiyo pamoja na kupewa msamaha wa kodi lakini cha kushangaza tangu mwaka 2015/16 hadi sasa haijarejesha kwa Manispaa ya Tabora fedha ilizolipwa kama kodi.

Kwa upande Mkurugenzi wa Manispaa hiyo Bosco Ndunguru alisema ni kweli kampuni hiyo ilileta gari moja likiwa ni bovu lakini malipo yake bado hawajamlipa hadi hapo atakapoleta gari jipya.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na wa Manispaa ya Tabora na viongozi mbalimbali leo ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake Mkoani humo.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akizungumza na watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tabora na wa Manispaa ya Tabora na viongozi mbalimbali leo ikiwa ni siku ya mwisho ya ziara yake Mkoani humo.

Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri akitoa maelezo mafupi leo kabla ya kumkaribisha Waziri Mkuu kwa ajili ya kuzungumza na watumishi na viongozi mbalimbali wa Manispaa na Ofisi yake.

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akizungumza na watumishi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Tabora (Kitete) leo mara baada ya kukagua majengo Chuo cha Afya. Wengine ni Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri(wa pili kutoka kulia) , Mkuu wa Wilaya ya Tabora Erick Komanya (kulia) , Mganga Mkuu wa Mkoa wa Tabora Dkt. Gunin Kamba(wa pili kutoka kushoto) na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi(kushoto)

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Kassimu Majaliwa akikiongozana na viongozi mbalimbali leo kukagua majengo ya Chuo cha Afya cha Tabora ambacho hakijaanza kutumika. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...