KAMPUNI ya Mega Beverage Company Limited,ya mkoani Arusha, inayotengeneza pombe kali chapa maarufu ya K Vant, imezindua chupa mpya za kinywaji cha K-Vant zenye mwonekano tofauti na chupa za awali.Mabadiliko hayo hayakubadilisha ladha halisi ya kinywaji hicho na wateja wake wataendelea kuifuahia ikiwa katika ladha yake halisi ya siku zote.

Lengo kubwa la kubadilisha chupa za pombe ya K-Vant, ni mkakati wa kampuni wa kupanua masoko yake ya ndani na nje ambapo imelenga kuwa katika mwonekano bora zaidi bila kuathiri ladha halisi ya kinywaji hicho ambayo inapendwa na watumiaji wengi wa pombe kali nchini na nje ya mipaka ya Tanzania

Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, mwishoni mwa wiki ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Mh.Antony Mavunde.

Mh.Mavunde,alipongeza hatua ya kampuni kubuni mkakati wa kuongea soko la bidhaa na kuongeza kuwa masoko yakiongezeka ndivyo mapato ya serikali yanaongezeka kupitia kulipa kodi sambamba na kuongeza wigo wa ajira kutokana na kuhitajika nguvu kazi zaidi.

“Serikali ya awamu ya tano inao mkakati wa kuifanya Tanzania nchi ya viwanda,tutazidi kuboresha mazingira zaidi kwa wawekezaji katika sekta hii ili lengo la kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hii lifanikiwe haraka sambamba na kupunguza changamoto ya tatizo la ajira kwa vijana “,alisema.

Mkurugenzi wa Masoko wa Mega Beverage Company Limited, Marco Maduhu alisema, “Kauli mbiu yetu ya kinywaji cha K-Vant katika mwonekano mpya ni ’Ni Halali Yako’ kampuni imejipanga kuimarisha usambazaji wa bidhaa ya pombe ya K-Vant katika sehemu zote nchini ili watanzania waendelee kufurahia ubora wake kikiwa katika mwonekano wa chupa mpya na katika ladha ileile waliyoizoe kuipata siku zote”.
Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde (wa pili kulia) akionyeshwa na Meneja mauzo na Masoko wa Kampuni ya Mega Beverages, Marco Maduhu, Chupa mpya ya K-Vant wakati wa uzinduzi wa muonekano mpya wa chupa ya kinywaji cha K-Vant uliyofanyika katika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam. (Kushoto) ni Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hiyo, Francis Kimaro.
Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira Anthony Mavunde (kulia) Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni Mega Beverages, wazalishaji wa Kinywaji cha K-Vant ,Francis Kimaro(kushoto) na Meneja Mauzo na Masoko wa Kampuni hiyo ,Marco Maduhu, wakigongeana glasi ya K-VANT.
Naibu waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Anthony Mavunde (katikati) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya Viongozi na baadhi ya wafanyakazi wa Mega Beverages wakati wa uzinduzi huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...