Maafisa waendeshaji wawili wa Kampuni ya Udalali ya Majembe,  wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Septemba 4, 2018 wakikabiliwa na shtaka la kujifanya watumishi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).

 Wakili wa Serikali Christopher Msigwa amewataja washtakiwa hao mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Janeth Mtega kuwa ni Mussa Kanena (39) na Malaki Malima (40).

Akisoma hati ya mashtaka, Msigwa amedai Machi 19, 2018 jijini  Dar es Salaam, washtakiwa kwa nia ya kudanganya walijifanya kuwa ni watumishi wa umma walioajiriwa na  Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) wakati wakijua kuwa si kweli.

Hata hivyo, washtakiwa wote wawili wamekana kutenda kosa na ni  mshtakiwa Malaki pekee aliyefanikiwa kukamilisha masharti ya dhamana, ila ametakiwa kuwasilisha hati ya kiapo itakayotambulisha majina yake ya Mark Malaki Malima na Malaki Malima kufuatia mdhamini wake kuwasilisha barua ya dhamana iliyokuwa na jina la Mark Malaki Malima huku katika hati ya mashtaka ikiionyesha Malaki Malima.

Mshtakiwa alipoulizwa juu ya majina hayo alidai yote ni majina yake hivyo ametakiwa kupeleka hati ya kiapo kuonyesha hayo yote ni majina yake.

Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo, bado haujakamilika.

Mshtakiwa Mussa amepelekwa rumande kwa kushindwa kutimiza masharti hayo ya dhamana.

Katika masharti ya dhamana, washtakiwa waliamuriwa kila mmoja kuwa na mdhamini mmoka atakayesaini bondi ya Sh milioni 2.

Kesi imeahirishwa hadi Septemba 18,mwaka huu.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...