Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
BAADA ya kusota rumande kwa takribani wiki mbili, leo Septemba 20.2018 askari mgambo wawili kati ya watatu wanaotuhumiwa kumpiga raia Robinson Olotu wameachiwa kwa dhamana baada ya mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kutoa masharti ya dhamana.

Washtakiwa wawili  Goodluck Tarimo (30) na Ofisa Mtendaji wa kata hiyo ya Bunju Ibrahim Mabewa (39) ndio wametimiza masharti ya dhamana huku mshtakiwa Kelvin Sawala akishindwa kutimiza masharti na kurudishwa rumande.

Hatua hiyo imekuja kufuatia wakili wa Utetezi Nassoro Mbilikira kuiomba mahakama iwapatie dhamana washtakiwa hao kwa sababu shtaka linalowakabili linadhaminika kisheria. 

Akisoma masharti ya dhamana,  Hakimu mkazi Mwandamizi Salum Ally amesema kila mshtakiwa anatakiwa kuwa na mdhamini mmoja anayetambulika kisheria atakayesaini bondi ya Sh. 500,000.

Mapema wakili wa serikali Nasoro katuga alidai mahakamani hapo kuwa, kesi hiyo leo imekuja kwa kutajwa upelelezi bado haujakamilika. . 

Watuhumiwa  hao ni miongoni mwa watu waliokuwa wakisimamia operesheni ya usafi iliyoasisiwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.

Washtakiwa hao wanadaiwa Agosti 30 mwaka huu maeneo ya Bunju Kinondoni jijini Dar es Salaam walimjeruhi kwa rungu Oloth.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 4 mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...