SERIKALI imeridhishwa na mradi wa mapinduzi katika sekta za kilimo na mifugo baada ya mradi huo unaotekelezwa katika halmashauri nne za Mkoa wa Mwanza kuonyesha mafanikio na tija kwa wakulima na wafugaji.

Akizungumza katika mahojiano na waandishi wa habari wilayani Misungwi hivi karibuni Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Rais(TAMISEMI) John Cheyo alisema baada ya kukutana na wakulima walikiri kuwa mradi huo una tija.

“Tulipokutana na wakulima maeneo mbalimbali ya mradi walikiri una tija na hivyo tukiuhamisha na kuupeleka katika mikoa mingine kunaweza kuwa mabadiliko makubwa zaidi kwenye kilimo. Ili kuongeza uzalishaji wakulima wanatakiwa kusaidiwa utaalamu na ushauri wa kupanda mbegu kwa nafasi na matumizi bora ya pembejeo,” alisema Cheyo.

Alifafanua kuwa mradi huo unafanya kazi kwa kushirikiana na serikali ya Mkoa wa Mwanza kwenye maeneo manne kujaribu zao la alizeti huko Buchosa na Sengerema ambako lilikuwa halijaanza ili wawasaidie wakulima walime kibiashara na kuongeza kipato, pia  Dalberg inajaribu kuongeza nguvu kwenye zao la pamba liwe na tija zaidi.

Mradi huo pia unawajengea uwezo maofisa ugani na mifugo kwa kuwapa kompyuta, vifaa vya kazi na  usafiri ili kufuatilia na kukusanya taarifa, kutunza takwimu na kumbukumbu kwa kutumia kompyuta.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mradi Dalberg Tanzania Steve Kisakye alisema kuwa mwaka 2016 serikali kupitia sekta ya kilimo na mifugo ilianza kufanya kazi na Dalberg 3D ikijikita kwa kutoa mafunzo na ufadhili wenye tija kwenye kilimo na ufugaji katika kuongeza uwezo kwenye sekta hiyo.
 Baadhi ya wakulima wilayani Sengerema wakiwa katika moja ya shamba darasa la zao la pamba walilolianzisha baada ya kupata elimu kwa ufadhili wa mradi wa Dalberg 3D.
 Afisa Mfugo Wilaya ya Misungwi  Dk. Chrispine Shami (mbele), Mratibu wa Dalberg wilayani humo Ines Muganyizi wakimuongoza  Mkurugenzi wa Uratibu (TAMISEMI)Dk. Andrew Komba (wa tatu nyuma)kukagua mashamba ya mfano ya  utekelezaji wa mradi wa Dalberg  3D wilayani humo.
 Mfugaji  wilayani Misungwi ambaye jina lake halikupatikana mara akiswaga ng’ombe wake kuingia ndani ya josho kwa ajili ya kuwaogesha dawa ya kuua wadudu. Josho hilo ni moja kati ya majosho yaliyofufuliwa kwa ufadhili wa mradi wa Dalberg 3D unaotekelezwa katika halmashauri nane za Mkoa wa Mwanza ambapo wameanza kuzingatia elimu ya ufugaji wanayopewa na wataalamu wa mifugo kupitia mradi huo. 
 Mkurugenzi wa mradi wa Dalberg Tanzania Steve Kisakye (kushoto) akitoa maelezo kwa Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Rais(TAMISEMI) John Cheyo (katikati)kabla ya kukabidhi pikipiki za usafiri kwa maofisa ugani na mifugo katika Wilaya ya Sengerema.Kulia ni Mkuu wa Wilaya hiyo Alfred Kipole.
 Mkurugenzi wa Dalberg Steve Kisakye (kushoto) akimkabidhi Mkurugenzi wa Sera na Mipango Ofisi ya Rais (TAMISEMI) John Cheyo pikipiki kwa ajili ya usafiri wa maofisa Kilimo (ugani) na Mifugo katika Wilaya ya Sengerema  ili ziwarahisishie usafiri wa kwenda vijijini kutoa elimu kwa wakulima na wafugaji pamoja na kukusanya taarifa.

KUSOMA ZAIDI  BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...