Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan leo amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke.

Pamoja na mambo mengine Balozi wa Uingereza nchini Tanzania Mhe. Sarah Cooke alimpa taarifa Makamu wa Rais juu ya ziara ya Mwanamfalme William wa Uingereza, atakayewasili nchini wiki ijayo kwa ziara yake ya siku tatu yenye lengo la kujifunza mambo ya uhifadhi wa wanyamapori kama sehemu ya maandalizi ya Mkutano wa Dunia unaohusu masuala ya Uhifadhi wa Wanyamapori utakaofanyika London, Uingereza mwezi Oktoba. 

Aidha Balozi Cooke alimjulisha Mhe. Makamu wa Rais utekelezaji wa makubaliano mbalimbali yaliyofikiwa kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi za Jumuiya ya Madola uliofanyika Aprili 2018, jijini London, Uingereza.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akizungumza na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam. (Picha na Ofisi ya Makamu wa Rais)
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akimsikiliza  Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke(kushoto) alipokuwa anafanya mazungumzo naye leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.  
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan(kulia) akiwa kwenye picha ya pamoja na Balozi wa Uingereza nchini Mhe. Sarah Cooke leo ofisini kwa Makamu wa Rais, Ikulu jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...