NA IS-HAKA OMAR, ZANZIBAR.

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein amesema mafanikio yaliyopatikana katika Sekta ya Elimu nchini yanatokana na Utekelezaji mzuri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015/2020.

Kauli hiyo ameitoa wakati akiweka jiwe la msingi katika Skuli ya Sekondari ya Kinuni iliyopo Wilaya ya Magharibi ‘’B’’ Unguja, amesema ujenzi wa skuli hiyo ya Ghorofa ambayo ni ya kisasa ni hatua kubwa ya kimaendeleo katika sekta ya elimu.

Alisema CCM kupitia Ilani yake imeahadi kuimarisha Sekta ya Elimu kwa kuimarisha miundombinu ya upatikanaji wa elimu ikiwemo kujenga majengo ya kisasa yanayoendana na kasi ya maendeleo katika zama za sasa.
Alibainisha kuwa Serikali ya awamu ya saba inaendeleza kwa vitendo falsafa ya elimu bila ya malipo iliyoasisiwa na Marehemu Mzee Abeid Aman Karume kwa lengo la kukuza kiwango cha elimu.

Alisema serikali ya ASP ilitangaza elimu bure kwa lengo la kuwakomboa watoto wa Waafrika waliokoseshwa fursa ya elimu kwa makusudi na utawala uliokuwa ukitawala kabla ya Mapinduzi ya mwaka 1964.Dk.Shein alisema pamoja na maendeleo yanayopatikana katika sekta za elimu bado zipo changamoto zinazoendelea kutatuliwa zikiwemo upungufu wa madarasa, madawati pamoja na upungufu wa walimu hasa wa masomo ya Sayansi.

Alisema Zanzibar kwa sasa imepiga hatua kubwa ya kimaendeleo katika sekta ya elimu ikilinganishwa na kabla ya Mapinduzi kwani na skuli za msingi 62 na skuli za sekondari nne lakini kwa sasa idadi imekuwa ni kubwa hadi hatua ya kuwa na Vyuo vikuu vinavyozalisha wataalamu wa kada tofauti kila mwaka.

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifungua pazia kuashiria uwekaji wa jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar sherehe zilizofanyika leo,akiwepo na Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pemba Juma,[Picha na Ikulu.] 21/09/2018.
DSC_6117
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimsikiliza Mkandarasi wa Kampuni ya Ujenzi ya Salem Construction LTD Nd,Aziz M.Qurban (katikati) alipokuwa akitoa maelezo baada ya kuweka  jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi leo ,sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar.
DSC_6388
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akitoa hutuba yake kwa Wananchi na Wanafunzi   katika sherehe ya  uwekaji wa   jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,sherehe zilizofanyika leo sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar,(kulia) Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Amali Mhe.Riziki Pembe Juma(kushoto)Waziri Kiomgozi Mstaafu na Mbunge wa Jimbo la Kijito Upele Mhe.Shamsi Vuai Nahodha na Naibu katibu Mkuu CCM Zanzibar Dk.Juma Abdala Sadala(wa pili kushoto),[Picha na Ikulu.] 21/09/2018. 
DSC_6430
Baadhi ya Wanafunzi waliohudhuria katika sherehe ya uwekaji wa   jiwe la msingi ujenzi wa Skuli mpya Sekondari ya Kinuni Jimbo la Pangawe Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein alipokuwa akitoa hutuba yake kwa   Wanafunzi hao leo katika sherehe Skuli hapo, [Picha na Ikulu.] 21/09/2018.
DSC_6054
Miongoni mwa madarasa mapya ya Skuli ya Sekondari ya Kinuni  Wilaya ya Magharibi”B” Mkoa wa Mjini Magharibi,yaliyowekwajiwe la msingi na  Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  sherehe zilizofanyika leo sambamba na Skuli 9 za Sekondari za Zanzibar.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...