Naibu Meneja wa Bandari  Utekelezaji, Ahmed Mchalaganya, kulia akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Omary Mgumba jinsi TPA inavyohudumia shehena ya mizigo inayopita bandarini wakati wa ziara ya waziri huyo kukagua kazi zinazofanywa na kitengo cha Ukaguzi wa Mimeo na Mazao kilichopo Bandari ya Dar es Salaam jana. Kushoto ni Kaimu Afisa Mfawidhi, Ofisi ya Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo Bandarini
 Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Omary Mgumba akitoa maelekezo kwa maofisa wa kitengo cha Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo Bandarini wakati wa ziara ya waziri huyo kukagua kazi zinazofanywa na kitengo hicho bandarini. Kushoto ni Kaimu Afisa Mfawidhi, Ofisi ya Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo Bandarini.
 Afisa Mkaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo bandarini, Bw. Deogratias Mosha, kulia akitoa maelezo kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo, Omary Mgumba jinsi kitengo cha Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo kinavyofanya kazi zake bandarini wakati wa ziara ya waziri huyo kukagua kazi zinazofanywa na kitengo hicho kilichopo Bandari ya Dar es Salaam jana. Kushoto ni Kaimu Afisa Mfawidhi, Ofisi ya Ukaguzi wa Mimea na Mazao ya Bidhaa za Kilimo Bandarini.
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo,  Omary Mgumba akizungumza na Mkurugenzi Mkuu wa TPA, Mhandisi Deusdedit Kakoko mara baada ya kumtembelea ofisini kwake na baadae kufanya ziara bandarini kukagua kazi zinazofanywa na kitengo cha Ukaguzi wa Mimeo na Mazao kilichopo Bandari ya Dar es Salaam jana. 

Na Leonard Magomba
NAIBU Waziri wa Kilimo, Mh. Omary Mgumba amesema kwamba kuanza kufanyakazi kwa kituo cha kuwaweka wadau wa bandari pamoja (One Stop Centre) kutapunguza gharama za kufanya biashara nchini.

Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) imejenga kituo cha kuwaweka wadau wa bandari pamoja (One Stop Centre) ili kurahisisha utendaji kazi na kupunguza urasimu wa utoaji wa mizigo bandarini.


Akizungumza wakati wa ziara yake kukagua kazi zinazofanywa na kitengo cha Ukaguzi wa Mimeo na Mazao katika Bandari ya Dar es Salaam, Waziri huyo amesema kwamba kuna haja ya wadau wote kuanza kukitumia kituo hicho ili kuboresha huduma.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...