Uongozi wa Benki ya NBC umetembelea Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF na kufanya mazungumzo na Mkurugenzi Mkuu yenye lengo la kuendeleza na kukuza uhusiano mzuri uliopo baina ya Benki na shirika hilo.

Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Bwana Theobald Sabi katika mazungumzo alisema benki hiyo ni miongoni mwa taasisi ambayo serikali imeweka hisa zake na inajivunia kufanya kazi na NSSF,kwani alisema Benki yake inaendeshwa kisasa zaidi ambapo katika kuhakikisha wanahudumia wananchi kwa haraka NBC wana huduma ya “mobile banking” inayoweza kuwafikia wananchi wengi waliopo vijijini wakiwemo wastaafu wa NSSF.

Kwa upande wake Mkurugenzi mkuu wa NSSF Bwana William Erio aliishukuru NBC kwa kuifanya NSSF kuwa mteja wake mkubwa zaidi katika huduma za kibenki na kuwashukuru kwa kuwa tayari kutoa ushauri wa kitaalamu utakaohitajika na Shirika kwa sasa katika boresha huduma zao.

Hata hivyo Bwana Erio aliwahakikishia uongozi wa NBC kwamba ushirikiano uliopo utaendelea kuimarika chini ya uongozi wake na alissitiza kuhakikisha mifumo ya fedha za wananchama inaendelea kuwa salama na kutumika kwa maendeleo ya Taifa. Pia alishukuru NBC kwa kuendelea kutoa riba ya asilimia tano kwenye akaunti ya makusaanyo kutoka kwa wanachama wa NSSF.

NBC imekuwa Benki ya nne kuweza kutembelea katika Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo benki nyingine ni pamoja na CRDB,NMB na UBA ambazo wote kwa pamoja wamekutana na NSSF na kupanga namna ya kuimarisha uhusiano wa kibiashara.
Mkurugenzi mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF na ujumbe wake (kushoto) akiwa na ujumbe wa Menejimenti ya Benki ya Taifa ya Biashara nchini NBC(kulia) ulioongozwa na Mkurugenzi mtendaji Theobald Sabi wakifurahia jambo kwenye mazungumzo yao yaliyofanyika katika makoa makuu ya NSSF jijini Dar es salaam ambapo kwa pamoja wamekubaliana kuendeleza mahusiano yao ya kibiashara.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF) , Bwana William Erio( katikati) akiwa na Menejimenti ya Benki ya Taifa ya Biashara,kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa NBC Theobald Sabi na wajumbe nane wakiwa kwenye picha ya pamoja baada ya kumalizika kwa mazungumzo makuu ya NSSF jijini Dar es salaam.(Watatu kulia ni Mkurugenzi wa Fedha wa NSSF Bwana Gambamala Luchunga na wa kwanza kushoto ni Meneja kiongozi wa Masoko na Uhusiano wa NSSF Bi.Lulu Mengele.)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...