Na Stella Kalinga, Simiyu
Waziri wa nishati Dkt Medard Kalemani amemuondoa Meneja wa TANESCO wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw.Amos  Mtae katika nafasi ya umeneja baada ya kushindwa kusimamia usambazaji wa umeme kupitia Mradi wa Umeme vijijini (REA) wilayani humo na amemwagiza Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO kumpangia kazi nyingine.

Waziri KALEMANI amechukua hatua hiyo katika mkutano wa hadhara mjini Meatu  akiwa katika ziara yake ya kukagua  kazi zinazofanywa na wakandarasi wa mradi wa Umeme vijijini REA awamu ya tatu Septemba 20, 2018, ambapo anaanzia katika uzinduzi wa mradi wa umeme  katika ofisi ya kijiji cha Dakama wilaya ya Meatu.

Dkt. Kalemani ameoneshwa kutoridhishwa na kasi ya mkandarasi anayesambaza umeme wilayani Meatu ambaye ni kampuni ya White City, kutokana na kutokuonekana katika vituo na kutokuwa na vifaa vya kutosha na vituo vya kutosha.

“Kasi ya mkandarasi hapa ni mbovu niliteegemea nione wakandarasai wanachakarika maana kote nilikotoka nimekuta wanachakarika, pili nilitegemea nione yadi ya vifaa vya wakandarasi wetu”

“Huyu meneja ndiye msimamizi wa wakandarasi, namuuliza anasema hajui leo wakandarasi wako wapi sasa anasimamia nini? Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO pokea maelekezo, kuanzia sasa huyu Meneja wa TANESCO Wilaya mtoe, weka Meneja mwingine kuanzia kesho hapa, wananchi wanataka umeme hapa” alisema Dkt. Kalemani.

Katika hatua nyingine Dkt. Kalemani amewahakikishia wananchi wa vijiji 36 vya wilaya ya  MEATU kupata umeme kupitia Mradi wa Umeme Vijijini (REA) Awamu ya tatu na akawasisitiza kuwa umeme utakapowafikia wautumie kwa ajili ya maendeleo.
 Aliyekuwa Meneja wa Meneja wa TANESCO wilaya ya Meatu mkoani Simiyu Bw.Amos  Mtae (wa pili kulia) akitoa maelezo kwa Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Medard Kalemani (wa tatu kulia), wakati wa ziara yake wilayani humo Septemba 20, 2018.
  Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani akikata utepe kuashiria uzinduzi wa Umeme wa REA Awamu ya Tatu katika Kijiji cha Dakama wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani akiwaonesha wananchi wa Kata ya Mwamishali kifaa cha Umeme kiitwacho UMETA , alipozungumza nao wakati wa ziarayake wilayani Meatu mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
 Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Medard Kalemani(kulia) akiteta jambo na Mkuu wa  Mkoa wa Simiyu, Mhe. Anthony Mtaka wakati wa ziara yake wilayani Meatu Mkoani Simiyu, Septemba 20, 2018.
Baadhi ya wananchi wa Kata ya Mwamishali wilayani Meatu wakishangilia baada ya Waziri wa Nishati Dkt. Medard Kalemani kuwatangazia kuwa vijiji vyote katika wilaya yao vitapata umeme kupitia mradi waWakala wa Nishati  Vijijini (REA) Awamu ya tatu, baada ya uzinduzi wa zoezi hilo katika Kijiji cha Dakama wilayani Meatu, Septemba 20,2018.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...