WANAHISA wa benki ya Azania wameonyesha kuridhishwa na mwenendo, ufanisi pamoja na mafanikio ya benki hiyo licha ya uwepo wa changamoto kadhaa zinazoikabili sekta ya benki hapa nchini, huku wakionesha kuridhishwa zaidi na namna benki hiyo ilivyoweza kukabiliana na changamoto ya mikopo isiyolipika.(Non- performing Loans) 

Wakizungumza kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa benki hiyo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo, wadau hao wamesema baada ya kupitia ripoti ya mwaka ya mwaka 2017 kuhusu mwenendo wa biashara wa benki hiyo wamebaini kuwa benki hiyo imepiga hatua kubwa kwenye nyanja kadhaa ikiwemo ongezeko la rasilimali (asset growth), kukidhi matakwa ya sheria za kibenki pamoja na kufanikiwa kukwepaji changamoto ya mikopo isiyolipika.

“Kwa mujibu wa ripoti hii ongezeko la rasilimali yaani asset growth ni asilimia 15 na zaidi kinachovutia zaidi ni kuona kwamba benki yetu imejitahidi sana kukabiliana na tatizo la mikopo isiyolipika kwa kuwa na asilimia 8 tu ya mikopo na wito wangu kwa uongozi wa benki ya Azania ni kuhakikisha asilimia hizi zinashuka hadi kufikia chini ya asilimia 6,’’ alisema mmoja wa wanahisa hao Bw Misheck Ngatunga.

Awali, akisoma taarifa yake, Mkurugenzi Mtendaji wa Benki hiyo Bw Charles Itembe alisema ufanisi wa benki hiyo umethibitishwa zaidi mwaka huu baada ya kutoa gawio la kiasi cha Sh. Mil 633 kwa wanahisa wake ikiwa ni mara ya kwanza tangu benki hiyo ianzishwe mwaka 1995. Alisema mafanikio hayo ya kiutendaji yameiwezesha benki hiyo kupata faida baada ya kodi kiasi cha Sh Bilioni 1.81 kutoka hasara ya sh. Bilioni 6.04 iliyoikumba benki hiyo mwaka 2016.
 Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bw Charles Itembe, (kushoto) akizungumza na wadau wa benki hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa benki ya Azania uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Wengine ni pamoja na Makamu Mwenyekiti wa Bodi  ya wakurugenzi wa benki hiyo, Bw  Eliudi Sanga (katikati) na Mkurugenzi wa Masuala ya kisheria wa benki hiyo Bw Charles Mugila.
 Makamu Mwenyekiti wa Bodi  ya wakurugenzi wa benki ya Azania Bw  Eliudi Sanga (kushoto) akizungumza na wadau wa benki hiyo kwenye Mkutano Mkuu wa mwaka wa benki ya Azania uliofanyika jijini Dar es Salaam leo. Kushoto kwake ni Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Azania Bw Charles Itembe.
 Baadhi ya wadau wa benki ya Azania wakifuatilia mkutano huo. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...