Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii.
RAIA wa Malawi, Edward Banda (38), amefikishwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu akikabiliwa na shtaka la uhujumu uchumi kuwepo nchini bila kibali,kutoa taarifa za uongo kwa maofisa wa serikali na kujipatia kitambulisho cha mpiga kura kwa njia ya udanganyifu.

Akisoma hati ya mashtaka leo Septemba 22, wakili wa serikali Mwandamizi, Veronika Matikila, mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,, Wanjah Hamza amedai Septemba 18, mwaka huu katika kituo cha Daladala eneo la Kawe Wilaya ya Kinondoni mshtakiwa  alikutwa akiwa hana nyaraka za kumuwezesha kuwepo nchini.

Pia imedaiwa, kati ya Januari na Oktoba 2015 katika shule ya msingi Mbezi Beach jijini Dar es Salaam, mshtakiwa alitoa taarifa za uongo kwa maofisa wa serikali kuwa yeye ni mtanzania ili aweze apate kitambulisho cha mpiga kura.

Imeendelea kudaiwa, mshtakiwa katika kipindi h cha kati ya Januari na Oktoba 2015, huko katika eneo la shule ya Msingi ya Mbezi Beach kwa udanganyifu aliwadanganya maofisa wa Tume ya Uchaguzi (NEC) waweze kumuamini na kumpatia kadi ya mpiga kura namba 1-1001-8940-587-6.

Hata hivyo, mshtakiwa baada ya kusomewa mashtaka yake hayo, hakuruhusiwa kujibu kitu chochote kwa sababu Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu haina mamlaka ya kuisikiliza kesi hiyo hadi Mahakama Kuu.

Hata hivyo wakili huyo aliwasilisha hati kutoka kwa  (DPP) mahakamani hapo kwa Kuzuia dhamana ya mshtakiwa huyo.


Kwa mujibu wa upande wa mashtaka upelelezi katika kesi hiyo bado haujakamilika na imeahirishwa hadi Oktoba 4, mwaka huu kwa ajili ya kutajwa.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...