Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
SEKRETARIETI ya Maadili ya Viongozi wa Umma, imezitaka Asasi za Kiraia (Azaki) kuwa mabalozi wa maadili ya viongozi wa umma na utawala bora ili kujenga jamii yenye maadili.

Akizungumza wakati akifungua mkutano wa mafunzo kwa Asasi za Kiraia (Azaki) Katibu wa Usimamizi wa Maadili wa Sekretarieti hiyo, John Kaole, amesema lengo la mafunzo hayo ni kukuza uelewa wa wananchi kuhusu majukumu na kazi zinazofanywa na sekretarieti hiyo pamoja na masharti ya maadili ambayo viongozi wa umma wanapaswa kiyazingatia.

"Matarajio yetu kuwa mafunzo haya yatawawezesha kushiriki vyema katika kutoa elimu ya maadili na utawala bora kwa wadau wenu na wananchi katika kujenga jamii yenye maadili na ambayo haivumilii kamwe vitendo vya utovu wa maadili miongoni mwetu.

Amesema serikali inatambua mchango mkubwa wa asasi za kiraia katika kuchangia maendeleo endelevu na kukiri kuwa kupitia mwongozo kuhusu ushirikishwaji wenye ufanisi kati ya Serikali na Azaki wa mwaka 2010, ambao umejikita katika kukuza uelewa na kubadilishana uzoefu kama tunavyofanya katika mafunzo haya.

"Ni matumaini yangu kuwa tutatumia maudhui ya mwongozo huo kutoa maoni na ushauri wenye tija kuhusu namna bora ya kukuza na kusimamia maadili ya viongozi nchini" amesema Kaole.

Ameongoza kuwa uadilifu ni nyenzo muhimu ya kukuza utawala bora nchini licha ya kazi ya usimamizi wa uadilifu na kukuza maadili miongoni mwa jamii ni ngumu na yenye changamoto nyingi.

"Lakini iwapo sisi asote tutashirikiana kwa pamoja tunaweza kukabiliana na changamoto hizo na hatimaye kupunguza kwa kiasi kikubwa kasi ya mmomonyoko wa maadili nchini" amesema Kaole.
Katibu idara ya ukuzaji wa maadili wa Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi Waziri Kipacha akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufungua semina ya kuwajengea uelewa wafanyakazi wa asasi za kiraia hapa nchini kuhusu ukuzaji na usimamiaji maadili ya viongozi wa umma ili waweze kujihuwisha na masuala yanayohusisha na maadili ya uongozi kwenye kwenye programu za kutoa elimu kwa wadau wao na wananchi kwa ujumla.
John Kaole akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kufunguliwa semina ya maadili ya kuwajengea uelewa kwa wafanyakazi wa sekta za kiraia jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya wadau wa asasi za kiraia wakiwa kwenye semina ya kuwajengea uwezo wafanyakazi wa asasi za kiraia jijini Dar es Salaam.
Picha ya pamoja ya wadau wa asasi za kiraia mara baada ya kufungua semina ya mafunzo kwa wafanyakazi wa asasi za kiraia jijini Dar es Salaam leo.
Picha na Avila Kakingo,Globu ya jamii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...