Na Mwandishi
wetu, Globu ya Jamii
KAMATI Kuu
ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), imewavua nafasi zote za uongozi
na kuwaweka chini ya uangalizi kwa mwaka mmoja, Mbunge wa Ubungo, Saed Kubenea
na Mbunge wa Moshi Vijijini, Anthony Komu baada ya kukiri kuwa sauti zilisombaa
katika mitandao ya kijamii wiki iliyopita ni za kwao.
Sauti hizo
ni zile ambazo wabunge hao wanasikika wakipanga namna ya kumshughulikia Meya wa
Ubungo, Boniface Jacob huku Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe, akitajwa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Alhamini Oktoba 18, Naibu
Katibu Mkuu Bara, John Mnyika, amesema hatua hizo zimechukuliwa baada ya
wabunge hao kuhojiwa na kamati kuu na kukiri sauti hizo ambazo zilihusisha
mazungumzo ya kuashiria utovu wa nidhamu ndani ya chama hicho ni za kwao.
“Tumewapa
adhabu mbalimbali kwa mujibu wa kanuni 6.5 (d) za chama na kamati kuu iliwaita
wabunge hao kuja kujibu tuhuma na walifika na kuhojiwa na walikiri mbele ya
kamati kuu ya chama kuwa sauti zilizosikika ni zao.
“Tukafikia
maamuzi ya kuwapa adhabu mbalimbali pamoja na kuwavua uongozi tuliwapa onyo
kali na kuwataka waandike barua ya kuomba radhi kwa chama na kwa watu
waliotajwa katika sauti hizo,” amesema Mnyika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...