Msanii
Jerry Boniface maarufu kama Mesen Selekta akishirikiana na mdogo wake
Gutta waliweza kuwapagawisha mashabiki kwa mtindo wao Singeli. Msanii
huyo alidhihirisha ubora wake uliopelekea uwanja kutimka vumbi kwa
nyimbo zake za Kinanda, Kanyaboya, Dab Singeli na nk.
Mji wa Mtwara ulikuwa tofauti na miji mingine kutokana na wasanii kuimba pamoja na mashabiki.
Akizungumza
na waandishi wa habari Mesen Selekta alisema " Hii inanipa mzuka kwa
mashabiki kuukubali muziki wangu, nimeona jinsi shangwe la Tigo Fiesta
Vibe Kama Lote walivyolipokea wana Mtwara".
Msanii
mwingine aliyeiteka Mtwara alikuwa Farid Kubanda Fid Q aliwaamsha kwa
wimbo wake Fresh, ambao aliurudia mara mbili kutokana na kiu ya
mashabiki.
Kivutio
kingine kilikuwa kwa MaDj Zero na Mafuvu waliweza kupiga mziki kwa
zamu kama kwa kushindana hii iliweza kuleta ladha na Vibe la aina yake
kwa mashabiki.
Kila
Tamasha linapopita utafutwa msanii Chipukizi kupitia shindano la kusaka
vipaji vya wasanii maarufu Kama Tigo Fiesta Supa Nyota, na kwa mkoa huo
msanii, Siraji Mbuta kwa jina la kisanii Mbuta The Swagx aliibuka
kidedea kuwakilisha mkoa huo kwenye fainali mwezi ujao.
Kwa
upande wa wadhamini Kampuni ya Tigo, Meneja wa Kanda ya Pwani, John
Tungaraza alisema ‘Mbali na muziki, wateja wa Tigo pia wanaweza kuvuna
hadi mara mbili ya thamani kwa vifurushi vya intaneti watakavyonunua
kupitia *147*00#. Promosheni ya Data Kama Lote itahakikisha kuwa
mashabiki wanaweza kufuatilia habari na matukio yote ya msimu wa Tigo
Fiesta 2018 – Vibe Kama Lote; au kufurahia kuperuzi kwenye mtandao wenye
kasi zaidi wa 4G+,’ Tungaraza alisema.
Wateja
wote wa Tigo pia wanaweza kuvuna hadi TSH 10 millioni, zawadi za kila
wiki za TSH milioni moja, ama zawadi za kil asiku za TSH 100,000 kwa
kushiriki katika shindano la Tigo Fiesta 2018 – Chemsha Bongo. Ushiriki
katika shindano hilo unapatikana kwa kutuma neno MUZIKIkwenda 15571 au
kwa kutembelea tovuti ya http://tigofiesta.co.tz.
Walioshusha
vibe kama lote mjini Mtwara ni pamoja na kundi la Rostam (Roma and
Stamina), Fid Q, Zaid na Weusii (Joh Makini, Niki wa Pili na G-Nako)
ambao walikonga mioyo ya wapenzi wa muziki mjini Songea pia. Wengine ni
wasanii wa bongo flava Mesen Selekta na Foby, wakongwe Chegge, Barnaba
na Mr Blue, pamoja na akina dada Ruby na Lulu Diva.
TIketi
za Tigo Fiesta 2018 – zitakuwa zinapatikana kupitia Tigo Pesa
Masterpass QR kwa kupiga *150*01#, kuchagua namba 5 (lipia bidhaa), na
kuchagua namba 2 (lipa kwa Masterpass). Tuma kiasi husika kwenda namba
ya Tigo Fiesta 78888888.
Msanii Chege kutoka TMK Family akionesha uwezo wake wa kutawala jukwaa kwenye Tamasha
kubwa la Tigo Fiesta -Vibe Kama Lote lililofanyika uwanja wa Nang'wanda
Mjini Mtwara usiku wa kuamkia Jumatatu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...