Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,Amina Khamis Shaban amesema hakuna sababu yoyote ya Tasisi za Umma kuendelea kufanya Vibaya  katika maeneo ya Ununuzi na Ugavi hili hali bodi ya usimamizi wa masula hayo ipo.
Naibu katibu Mkuu amesema hay oleo Jijini Dar es Salaam alipokuwa akitoa hotuba kwa wahitimu wa Mahafali ya tisa ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi (PSPTB) yaliyofanyika katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.

“ninawaagiza kwa kushirikiana na tasisi zingine zinazosimamia ununuzi wa Umma kama  PPRA,GPSA,PPAA na zingine mlete mpango kazi namna mtakavyofikia tasisi za umma ili kupitia Wizara ya Fedha na Mipango tuweze kutekeleza jambo hili mapema iwezekanavyo.Lengo ni kuhakikisha tunatumia rasilimali zilizopo ili kuleta Matokeo Makubwa kwa Wananchi” Amesema Naibu Katibu Mkuu.

Kwa upande wake Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi, Godfred Mbanyi  amesema bodi itaendelea na jitihada zake kuhakikisha wahitimu wa fani ya ununuzi na ugavi wanakuwa na sifa stahiki ili kuweza kupenya na kuleta ushindani katika soko la ajira la ndani nan je ya nchi .

Mbanyi amesema bodi imeweza kuwatafutia fursa vijana wawili wa CPSP Na Wanafunzi bora wa somo la Procurement and Suply Audit nafasi ya ajira katika tasisi ya Kimataifa ya Nexia SJ Tanzania ambao ni Wataalamu wa Ukaguzi, Hesabu,Kodi, Ushauri wa Kibiashara nk.

Mbanyi alimaliza kwa kutoa rai kwa wahitimu wote watakaotunukiwa shahada ya juu ya fani ya ununuzi na ugavi wafanye hima kujisajili na bodi ili waweze kufanya kazi za ununuzi na ugavi kihalali na kwa mujibu wa sheria .

 Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,  Amina Khamis Shaban akihutibia wakati wa mahafli ya tisa ya Bodi ya Wataalmu wa Ununuzi na Ugavi(PSPTB) Katika Viwanja vya Karimjee Jijini Dar es Salaam.
 Kaimu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Wataalamu wa Ununuzi na Ugavi , Godfred Mbanyi akitoa hotuba yake kwenye Mahafali ya tisa ya bodi hiyo.
 Wahitimu wakila kiapo cha Uadilifu na Maadili mbele ya Mgeni rasmi mara baada ya  kutunikiwa shahada zao mbalimbali za masuala ya Ununuzi na Ugavi katika Viwanja vya Karimjee
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha na Mipango ,  Amina Khamis Shaban akiwa katika picha ya Pamoja na Wafanyakazi wa bodi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...