Na Mwandishi wetu
Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya amewataka wasichana nchini kujipanga vyema kutafuta maisha kwa kuzingatia fursa ambazo zipo.
Akizungumza baada ya kutembelea shule ya sekondari Jangwani ambayo na yeye alisoma katika miaka ya 1970 Mkurugenzi huyo alisema elimu ni mojawapo ya kitu muhimu katika kufanikisha malengo ya kuwa juu kiuchumi na kimadaraka.
Alisema nafasi za juu zinaweza kupatikana kwa kukazania elimu, kujituma kwa bidii na kujifunza kutoka kwa wengine hasa nchi zilizoendelea.
Alisema wakati yeye anasoma hapakuwepo na nafasi kubwa kwa wasichana lakini kwa sasa nafasi zipo wazi na wakijipanga vyema watakuwa miongoni mwa watu wanaoendesha uchumi na kutegemewa na familia zao.
Alisema kitu muhimu kwa wasichana waliopo sasa ni kujijenga kwa namna ambavyo wataweza kutumika vyema katika sekta zozote huku wakiendeleza uhusiano mzuri na familia zao ambazo ndio msingi wa mafanikio.
Katika mahojiano na waandishi wa habari baada ya ziara yake hiyo ya kutia hamasa wasichana wa Jangwani alisema mazingira magumu yaliyoelezwa na Mkuu wa shule ya sekondari Jangwani  ataangalia namna ya kusaidia ingawa si moja kwa moja kulingana na nafasi yake.
Katika mazungumzo Mkuu wa shule hiyo yenye wanafunzi 1,470 , mwalimu Bi. Nyaibuli Boke alisema shulehiyo inakabiliwa na changamoto za mabweni kwani lililopo linakidhi mahitaji ya walemavu kwa asilimia 75 huku asilimia zilizobaki ni za wanafunzi wa kawaida.
Aidha alisema wana uhaba wa vitabu vya mchepuo wa Sanaa a na pia zana za walemavu za kujifunzia zikiwa pungufu.
Pamoja na changamoto zilizopo ambazo zilisababisha shule hiyo kushuka ufaulu, mwalimu Boke ambaye amehamishiwa hapo mwaka huu akitoka sekondari ya King’ongo iliyopo manispaa ya Ubungo, alisema wamejipanga kurejesha heshima ya shule hiyo.
Alisema kumekuwa na kamati ya mitihani, kurejesha hamu ya ufaulu na pia kuwa na mazungumzo na wazazi kwa wale wanafunzi ambao wanaonekana hawafanyi vyema kujua matatizo na kusaidia kuyatatua.
Alisema wamekuwa wakishirikisha wazazi kufanikisha kampeni ya kuzingatia kauli mbiu ya divisheni ziro na 4 mwiko.
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya akizungumza na wasichana wa Shule ya Sekondari Jangwani kuwamasisha kufanya vyema kwenye masomo yao alipotembelea shuleni hapo kuwashukuru walimu kwani bila wao asingefika hapo wakati wa ziara yake nchini jana jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya wanafunzi wenye ulemavu wa viungo wakimsikiliza Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya (hayupo pichani) alipokuwa akiwapa hamasa ya kufanya vyema kwenye masomo yao ikiwemo na kujitambua wakati wa ziara fupi shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam.
 Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya katika picha ya pamoja na wasichana wa Shule ya Sekondari Jangwani mara baada ya kuwahamasisha na kuwatia moyo wakati wa ziara yake fupi shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam.
Mwalimu mkuu wa Shule ya Sekondari Jangwani, Bi. Nyaibuli Boke (wa pili kushoto), Afisa Elimu Sekondari wa Manispaa ya Ilala, Bi. Eliza Ngonyani (kulia) katika picha ya pamoja na Naibu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Mazingira (UNEP), Joyce Msuya (wa pili kulia) aliyeambatana na Afisa mwakilishi wa Shirika la Mazingira la Umoja wa Mataifa nchini, Bi. Clara Makenya (kushoto) alipofanya ziara fupi ya kutembelea shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam.


 KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...