Na Khadija Seif, Globu ya jamii
Ni furaha kwa kwenda mbele! Ndivyo unavyoweza kuielezea Bendi ya African Stars Twanga Pepeta ambayo mwaka huu imetimiza miaka 20 tangu kuanzishwa kwake. Sherehe za kusheherekea miaka ya uwepo wa bendi hiyo iliyosheheni wanamuziki maarufu na wenye vipaji katika muziki was dansi inatarajia kufanyika Oktoba 27 mwaka huu katika ukumbi wa Life Park zamani New World Cinema eneo la Mwenge  Jiji la Dar es Salaam.

Mkurugenzi wa Kampuni ya African Stars Entertainment (ASET) Twanga Pepeta  Iron Lady Asha Baraka ameeleaza leo   jijini Dar es Salaam namna ambavyo wamejipang kusheherekea miaka 20 tangu kuanzishwa kwa bendi hiyo.

"Katika sherehe hiyo  ya miaka 20 ya bendi yetu  itapambwa  na vipaji vipya kutoka kwa vijana wadogo kama Tarick  na Fetty Kalumba," amesema.

Amefafanua kuwa usiku wa sherehe hiyo kutakua na muda wa kuwaenzi waanzilishi pamoja na wasanii ambao wametangulia mbele ya haki kama Hamisi Amigoras, Abuu Semhando "Baba Diana", Banza Stone, MCD na wengine ambao wamefanya jitihada mpaka hapo bendi ilipofikia.

Asha Baraka ameongeza kwa siku ya kesho kazi zao zitaanza kusambazwa katika vituo vya habari ili kuhamasisha wapenda muziki. wadau pamoja na viongozi mbalimbali kwa lengo la kuwahamasisha kufika katika sherehe hiyo ya miaka 20 na vibao kama Povu, Rekebisha na vingine vitatumbuizwa kwa mara ya kwanza.
Kwa upande wake Kiongozi Mkuu wa bendi hiyo ambae pia  ni muimbaji wa siku nyingi Luiza Mbutu amewaahidi mashabiki na wadau mbalimbali wa muziki wa dansi kujitokeza kuwaunga mkono kwa hali na mali ili kufanikisha sherehe hizo.
Pia amesema sanjari na hilo  watatembelea kituo cha watoto ya yatima kilichopo  Kinondoni Moscow kwa ajili ya kutoa misaada mbalimbali kama kurudisha fadhila kwa jamii pamoja na kuwatembelea  wagonjwa katika Hospitali ya  Mwananyamala iliyopo Kinondoni jijini Dar es Salaam.

Pia amesema waendesha bodaboda watapewa reflecta kwa ajili ya kumuenzi Mwanamuziki Abuu Semhando ambae alipata ajali ya pikipiki.

Wakati huo huo Hassan Mussa 'Super Nyamwela' ambaye ni  Kiongozi wa wanenguaji amessema wamejipanga kuhakikisha wanatoa burudani ya aina yake ambayo itakonga nyoyo za mashabiki, wapenzi na wadau wa bendi hiyo na muziki maarufu nchini. Amesema umahiri na uhodari wake katika kunengua na kumiliki jukwaa uko palepale au zaidi na kwamba jukwaa la wanenguaji zaidi ya 18 watakuwa jukwaani siku ya sherehe hizo.

Amesema katika idara ya ushereheshaji  kuna baadhi ya wanenguaji ambao wamekuwa bado wanaigaiga baadhi ya miondoko hivyo wanakaribishwa kwenye sherehe ya kuzaliwa kwa bendi ya  Twangapepeta  kwani ndio kisima cha burudani.
Msanii mpya ambaye ametambulishwa rasmi kwenye bendi hiyo Fetty Kalumba  ambaye amesema amejipanga vizuri kwenye kusherehesha usiku huo na kuhimiza wapenzi wa Twanga kufika na kujumuika pamoja.
 Kiongozi na Muimbaji wa bendi ya Twanga Pepeta Luiza Mbutu akitambulisha baadhi ya vipaji vipya vitakavo tumbuiza usiku wa miaka 20 ya bendi hiyo itakayofanyika katika ukumbi wa Life Park. wa kwanza kulia ni Mkurugenzi wa bendi ya African Stars Asha Baraka.
Mnenguaji Mkuu wa bendi ya Twanga Pepeta Hassan Mussa 'Super Nyamwela'  akizungumza na waandishi wa habari kuhusu maadhimisho ya miaka 20 ya kuanzishwa kwa bendi hiyo itakayofanyika ukumbi wa Life Park Jijini Dar es Salaam.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...