Na Ripota Wetu,Globu ya jamii
WAKILI Augustine Shio anayemtetea Mwenyekiti wa Usajili wa klabu ya Simba Sc Zacharia Hans Poppe ameieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es salaam kuwa mteja wake alikuwa yupo nchini Marekani

Ameyaeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Thomas Simba, wakati akimuombea dhamana mteja wake. 
Wakili Shio ameeleza kuwa Hans Poppe alikuwa nchini Marekani kwa matibabu lakini aliamua kukatisha matibabu hayo na kurudi nchini kusikiliza tuhuma zinazomkabili.
Amedai kuwa Hanspope alimuandikia barua na kumjulisha kuwa anarudi nchini Oktoba 15 mwaka 2018 na kumtaka awajulishe Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) kuhusu ujio wake.
Wakili Shio amedai, aliwafikishia ujumbe Takukuru ndipo usiku wa jana Oktoba 15 2018, ambapo saa 7:25 usiku Hans Poppe aliwasili na alipofika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere alikamatwa na TAKUKURU  lakini baadaye waliweza kumruhusu alale nyumbani kwake na asubuhi walimfikisha mahakamani.

Hans Poppe kwa sasa yupo nje kwa dhamana, huku wenzake wawili ambao ni Rais wa Klabu ya Simba Evans Aveva na Makamu wake Godfrey Nyange wanaendelea kusota mahabusu kwa kuwa mashtaka yao hayana dhamana.


Mtuhumiwa Haspope akitoka nje ya mahakama ya hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam leo mara baada ya kusomewa mashtaka yanayomkabiri na baadaye kuachiliwa kwa dhamana.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...