Na Karama Kenyunko blogu ya jamii.

MAHAKMA ya Hakimu Mkazi Kisutu leo Novemba 19.2018 imemuonya mshereheshaji maarufu nchini, Anthony Luvanda maarufu kama MC Luvanda kwa kitendo chake cha kusafiri bila ya ruhusa ya Mahakama.

Onyo hilo limetolewa na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi wakati kesi dhidi ya mshtakiwa hiyo ilipoitwa mahakamano hapo kwa ajili ya kutajwa.

Hatua hiyo imefikiwa badaada ya wakili Kishenyi kuieleza mahakama kuwa upelelezi wa kesi hiyo bado haujakamilika na kwamba mara ya mwisho kulikuwepo na amri ya mahakama ya kumkamata mshtakiwa huyo kwa kusafiri bila ruhusa ya mahakama.Wakili Kishenyi akaongeza, kwa sababu mshtakiwa amejitokeza mwenyewe akumbushwe masharti ya dhamana.Kufuatia maelezo hayo, wakili anayemtetea Luvanda, Jebra Kambole alidai hana pingamizi kuhusu mshtakiwa kukumbushwa masharti ya dhamana na akaomba radhi kwa yaliyotokea na kwamba mambo hayo hayatajirudia tena.

Hakimu Shaidi alimwambia mshtakiwa kuwa kila kitu kinanidhamu yake, hata katika kesi na kufika mahakamani kuna nidhamu yake lakini kitendo cha wewe kusafiri bila kuitaarifu mahakama siyo kitu kizuri, ukitaka kusafiri toa taarifa.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Desemba 18, mwaka huu na akamuonya mshtakiwa huyo afuate utaratibu.Katika kesi hiyo, MC Luvanda pamoja na kampuni yake, Home of Company Limited. wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kutumia kikoa ambacho akijasajiliwa Tanzania huku Luvanda akishtakiwa kwa kosa la kutoa maudhui mtandaoni bila ya kuwa na kibali cha Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA).

Inadaiwa kuwa kati ya Februari 24 na Septemba 2018 katika jiji la Dar es Salaam, mshtakiwa huyo alianzisha na kutumia mtandao wa www.mcluvanda.com ambao haukuwa na kikoa cha .tz.Aidha imedaiwa,mshtakiwa huyo alitoa Huduma ya online kupitia online TV ifahamikayo kama MC Luvanda pasipokuwa na kibali toka TCRA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...