WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amesema Jeshi la Polisi lipo imara kupambana na uhalifu wa aina yoyote utakaojitokeza nchini hivyo wahalifu wasithubutu kulichezea, wala ‘kulibipu’.

Lugola pia amewataka wananchi kuendelea kuwapa taarifa za uhalifu Polisi ili ziweze kufanyiwa kazi haraka kwa kuwa Serikali ya Rais Dk. John Magufuli si ya kuchezewa na imejipanga kikamilifu kwa kuwalinda wananchi wake.

Akizungumza katika mkutano wa hadhara na wananchi wa Kijiji cha Ragati, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, Lugola alisema Jeshi la Polisi lipo imara na litaendelea kuwalinda wananchi pamoja na mali zao, ila Polisi ili waweze kufanya kazi zao kwa umakini zaidi, wananchi wanapaswa kuwasaidia katika kufichua uhalifu katika maeneo yao wanayoishi.

Lugola aliyazungumza hayo baada ya wananchi wa Kijiji hicho kumlalamikia kuwa kuna kundi la vijana ambalo linaongozwa mwananchi mmoja kijijini hapo wanahatarisha amani na kuwafanya kuishi kwa wasiwasi na kushindwa kufanya shughuli zao za maendeleo.

“Polisi wapo kwa ajili yenu hivyo kuweni huru muda wowote kutoa taarifa za kiuhalifu katika maeneo yenu, hivyo kutokana na viashiria hivyo vya uvunjifu wa amani katika Kata hii namuagiza mkuu wa polisi wilaya (OCD) kuwasaka, kuwakamata wale wote ambao wanahatarisha amani katika Kata hii ya Kasuguti,” alisema Lugola. Lugola aliongeza kuwa, yeye ni Mbunge wa Jimbo hilo na pia ni Waziri ambaye anasimamia usalama wa wananchi na mali zao, hivyo hatakubali wananchi waishi kwa wasiwasi katika maeneo yao na nchi kwa ujumla, na pia Serikali ya Magufuli haichezewi, haijaribiwi na wala haibipiwi na mtu yeyote.

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kulia), akimsindikiza kumpeleka ndani ya gari Mkazi wa Kitongoji cha Songambele, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara mwenye umri wa miaka 100, Mzee Mtatiro Silla, mara baada ya Waziri huyo kumaliza mkutano wake wa hadhara akizungumza na wananchi wa Kata hiyo, Wilaya ya Bunda, Mkoani Mara, leo. Lugola aliwataka wananchi jimboni kwake watoe polisi taarifa za uhalifu nchini na pia Serikali ya Awamu ya tano ipo imara haichezewi na mtu yeyote. Pia Lugola aliwataka wananchi jimboni kwake waanze maandalizi ya kilimo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Mkazi wa Kitongoji cha Songambele, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara, mwenye umri wa miaka 80, Mzee Nyamuhanga Mtatiro Silla, wakati mzee huyo alipokua anamuuliza swali Waziri Lugola katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika kitongoji hicho, leo. Wapili kushoto meza kuu ni Mzee mwenye umri wa miaka 100, Mtatiro Silla ambaye ni baba mzazi wa anayezungumza, na mtoto wake wa tatu katika kuzaliwa. Baba na mwana wote walihudhuria mkutano huo wa Waziri Lugola. Lugola aliwataka wananchi jimboni kwake watoe polisi taarifa za uhalifu nchini na pia Serikali ya Awamu ya tano ipo imara haichezewi na mtu yeyote. Pia Lugola aliwataka wananchi jimboni kwake waanze maandalizi ya kilimo. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mwibara, Kangi Lugola (kushoto), akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Kasuguti, Kata ya Kasuguti, Jimbo la Mwibara, Mkoani Mara, akiwataka wananchi jimboni kwake watoe taarifa za uhalifu Polisi na iliwawe na amani na waendelee kufanya shughuli zao za kilimo, pia alisisitiza kuwa Serikali ya Awamu ya tano ipo imara haichezewi na mtu yeyote.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...