Serikali
imeitaka kampuni ya Acacia kuandaa na kuwasilisha haraka mpango mpya wa
urejeshaji mazingira katika hali yake ya kawaida baada ya kusitisha shughuli za
uchimbaji dhahabu katika mgodi wa Buzwagi uliopo wilayani Kahama ifikapo mwaka
2020.
Naibu Waziri
wa Madini, Doto Biteko aliyasema hayo jana alipofanya ziara katika mgodi huo
kukagua shughuli zinazoendelea mgodi hapo.
Mapema mwaka
huu, Wizara ya Madini iliukataa mpango uliokuwa umeandaliwa na kampuni hiyo
ukikadiriwa kutumia dola milioni 18 kwa kuwa haukujumuisha kufukiwa baadhi ya
mashimo mgodini hapo (tazama picha), bali yabaki wazi hadi yatakapojaa maji
katika kipindi cha miaka 100 ijayo.
Naibu Waziri Doto Biteko (katikati), akifafanua jambo wakati akikagua shughuli mbalimbali katika mgodi wa Buzwagi.
Naibu Waziri Doto Biteko akielekea kukagua sehemu ambapo mchanga wenye madini (makinikia) umehifadhiwa ndani ya mgodi wa Buzwagi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...