Na: Frank Mvungi- MAELEZO

Msajili wa Hazina Bw. Athumani Selemani Mbuttuka amewata Watendaji wakuu , Wenyeviti na Wajumbe wa Bodi za Taasisi na mashirika ya umma kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia Sheria, Kanuni, Taratibu na miongozo inayotolewa na Serikali .

Akizungumza katika Semina ya kuwajengea uwezo Viongozi hao, Bw. Athumani amesem,a kuwa lengo la Serikali ni kuona dhamira ya kuazishwa kwa Taasisi na Mashirika ya Umma inafikiwa kwa wakati.

“Kwa mujibu wa vifungu Na.10 (2) (e) na 10 (5) vya Sheria ya Msajili wa Hazina ina mamlaka ya Kusimamia Bodi za Taasisi na Mashirika ya Umma hivyo, tuna wajibu wa kuhakikisha kuwa Bodi na Viongozi wote wanaelewa majukumu yao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu”; Alisisitiza Mbutuka.

Akifafanua amesema kuwa Bodi na Watendaji wakuu wanapaswa kuwa makini, wabunifu na kufanya maamuzi sahihi na kwa wakati ili kuhakikisha kuwa Taasisi zinajiwekea mikakati ya kupunguza gharama za uendeshaji zinazotokana na matumizi yasiyo ya lazima hususani safari za Bodi na viongozi zisizokuwa na manufaa kwa Taasisi husika.

Alibainisha kuwa Taasisi zinapaswa kuwa na mikakati madhubuti ya kukusanya mapato ili kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi, sambamba na kuhakikisha kuwa matumizi yote yanafanyika kwa kuzingatia Sheria, Kanuni na miongozo mbalimbali ya Serikali.

Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina kwa Watendaji Wakuu, Wenyeviti na wajumbe wa Bodi kuhusu usimamizi wa Taasisi na mashirika ya Umma ili kuyawezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake. 
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Maendeleo ya Biashara Tanzania Bw. Edwin Rutageruka akizungumza wakati wa semina kwa Watendaji Wakuu, Wenyeviti na wajumbe wa Bodi kuhusu usimamizi wa Taasisi na mashirika ya Umma ili kuyawezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake, Semina hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Msajili wa Hazina. 
Msajili wa Hazina Bw. Athumani Mbuttuka (katikati)akiwa kwenye picha ya pamoja na sehemu ya watendaji wakuu wa mashirika ya umma walioshiriki katika semina kwa Watendaji hao, Wenyeviti na wajumbe wa Bodi kuhusu usimamizi wa Taasisi na mashirika ya Umma ili kuyawezesha kutimiza malengo ya kuanzishwa kwake. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...