Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

BENKI Kuu ya Tanzania (BoT) tawi la Dodoma limefafanua kwa kina majukumu yake mbalimbali na miongoni mwa majukumu hayo ni kutunza na kusambaza fedha (noti na sarafu) safi za thamani mbalimbali kwa ajili ya kuwezesha wananchi kutekeleza shughuli mbalimbali za uchumi katika Kanda ya kati. 

Tawi la BoT, Kanda ya Kati, Dodoma, ni tawi la tano kufunguliwa tangu nchi ipate uhuru; na ni moja ya matawi mawili ambayo yamefunguliwa miaka ya hivi karibuni.Wakati tawi la Dodoma limefunguliwa 15/10/2015, Tawi la Mtwara limefunguliwa Machi 2017. 

Awali Tawi la Dodoma lilitarajiwa kutoa huduma za benki kuu katika mikoa ya Dodoma, Singida Iringa and Tabora. Hata hivyo kutokana na kukamilika ujenzi wa tawi la Mtwara, na kama ilivyokuwa kwa matawi mengine ya awali, mgawanyo wa mikoa katika kanda za Benki Kuu ulibadilika. 

Meneja wa masuala ya Fedha na Takwimu kutoka Benki Kuu ya Tanzania(BoT) tawi la Dodoma Dk.Camilius Kombe ametaja baadhi ya majukumu ya tawi hilo wakati anazungumzia majukumu ya benki hiyo kwa waandishi wa habari waliokuwa kwenye mafunzo ya habari za fedha na uchumi.

Ambapo katika majukumu hayo yapo pia ya kukusanya fedha zilizotumika kutoka vituo maalum vya kusambazia fedha vilivyo katika baadhi ya mabenki ya biashara na kuondoa katika mzunguko fedha ambazo zimechakaa na hazifai kutumika tena.
Meneja Msaidizi wa Idara ya Uhusiano na Itifaki katika Benki Kuu ya Tanzania(BoT) akifafanua jambo kuhusu namna ya kutambua fedha bandia kwa waandishi wa habari za Fedha na Uchumi baada ya kutembelea BoT tawi la Dodoma kuangalia namna wanavyotunza fedha.
Baadhi ya maofisa wa Benki Kuu ya Tanzania wakisoma kitu kwenye Kompyuta mpakato wakati wa semina ya mafunzo ya uandishi wa habari za fedha na uchumi ambapo waandishi mbalimbali wa vyombo vya habari nchini wanashiriki semina hiyo inayoendelea Mjini Dodoma
Meneja Msaidizi kutoka Kurugenzi ya Fedha Benki Kuu ya Tanzania(BoT) tawi la Dodoma Nolasco Maluli akizungumzia majukumu ya tawi hilo wakati wa semina ya waandishi wa habari mjini Dodoma leo
Meneja Msaidizi wa Huduma za kibenki BoT tawi la Dodoma Lilian Silaa akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani wakati wa semina ya mafunzo ya uandishi wa habari za fedha na uchumi
Mtangazaji na Mwaandishi wa redio Clouds FM akizungumza kwenye semina ya waandishi wa habari za fedha na uchumi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...