Shindano hilo lililodumu kwa kipindi cha miezi mitatu lilikuwa na lengo la kutoa elimu ya stadi za biashara na fedha kwa wafanyabiashara wadogo. 

Benki ya FINCA Microfinance imeendelea kuwa benki ambayo inaunga mkono ushirikishwaji wa kifedha katika kipindi cha miaka 20 na zaidi cha uwepo wake nchini Tanzania. Bugingo Emmanuel ameibuka mshindi wa shindano la biashara la Kuza Ofisi na FINCA na kuondoka na kiasi cha TZS milioni 10 baada ya shindano la muda wa miezi mitatu na lililokuwa na zaidi ya washiriki elfu moja walioshiriki, ni washriki wanne ndio waliowasilisha mipango yao ya biashara kwa jopo la majaji na kupigiwa kura na watazamaji. 

Akiongea katika onyesho la mwisho la shindano la Kuza Ofisi na FINCA jijini Dar es salaam, Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde aliipongeza FINCA kwa kutekeleza jitihada za kibunifu kwa ajili ya kusaidia kukuza wajasiriamali wadogo kwa wakati. Alisema kwamba serikali inaendelea kuandaa mazingira mazuri kwaajili ya maendeleo ya biashara nchini.

“Ninatoa wito kwa vijana kuchangamkia fursa zinazotolewa na mifuko ya uwezeshaji ya serikali ambayo imetengwa kwaajili ya maendeleo ya biashara. Vile vile aliipongeza benki ya FINCA Microfinance kwa jitihada zake zenye lengo la kusaidia kukuza wafanyabiashara wadogo SMEs nchini ‘Ninaipongeza FINCA kwa kubuni mipango hii ya kibunifu ambayo sio tu kwamba inasaidia kukuza biashara ndogo ndogo lakini pia inawapatia vijana ujuzi na stadi za biashara alisema Mavunde. 
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (katikati) akikabidhi mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi milioni 10 jana kwa mshindi wa shindano la Kuza Ofisi na FINCA, Emmanuel Bugingo mkazi wa Mbagala Kuu. Shindano hilo lililoandaliwa na Benki ya Finca Microfinance linashindaniwa kwa washiriki kubuni mradi wenye kuweza kumletea kipato kwa kupitiwa na majaji waliompata mshindi. Pichani Kushoto ni Afisa Mkuu Uendeshaji wa Benki ya Finca Microfinance, Alfred Vanderlin. 
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana, Ajira na Walemevu, Mhe. Anthony Mavunde akitangaza mshindi wa shindano la Kuza Ofisi na FINCA lililofikia kilele jana usiku kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar Es Salaam, Shindano lililoendeshwa kwa miezi mitatu kwa washiriki kubuni mradi chanya wenye kumuwezesha kupata kipato. Wengine pichani kushoto ni Afisa Mkuu Uendeshaji wa Benki ya Finca Microfinance, Alfred Vanderlin na washiriki walioingia nne bora. 
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mhe. Anthony Mavunde (katikati) akikabidhi mfano wa Hundi yenye thamani ya shilingi milioni 5 jana kwa mshindi wa pili wa shindano la Kuza Ofisi na FINCA, Sadiki Hassani mkazi wa Manzese, Kushoto ni Alfred Vanderlin, Afisa Mkuu Uendesheji wa Finca. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...