Na mwadishi wetu,Arusha .

Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF)umewataka wanachama wa Vyama vya Msingi vya Ushirika wa Mazao kujiunga na Bima ya Afya kwaajili ya kupata matibabu bora ambao ni mpango wa serikali ya awamu ya tano ifikapo mwaka 2020 idadi kubwa iwe imejiunga na mfuko huo.

Meneja wa NHIF mkoa wa Arusha,Isaya Shekifu amesema Ushirika Afya ni mpango mahususi ulioanzishwa na serikali kwa lengo la kutoa huduma ya bima ya afya kwa wakulima kupitia vyama vya ushirika vya msingi kwa kuanzia na mazao matano. Ameyataja mazao hayo matano ya kimkakati kuwa ni Korosho,Pamba,chai,Kahawa na Tumbaku ambayo baada ya kuzinduliwa kwa mpango huo na Waziri Mkuu,Kassim Majaliwa mwaka huu mfuko ulianza kutoa huduma za matibabu kwa wakulima.

Shekifu amesema mkulima anatakiwa kulipa kiasi cha Sh 76,800 ukiwa ni mchango wake kwaajili ya kupata Ushirika Afya na itamwezesha kupata huduma ya matibabu kwa mwaka mzima pia ataruhusiwa kuwakatia bima hiyo kwa mwenza,mzazi,mkwe na watoto. Mrajisi wa Ushirika mkoa wa Arusha,Emmanuel Sanka amesema mpango huo utasaidia wanachama wake kunufaika na matibabu yanayotolewa na mfuko huo hatua itakayoongeza tija katika shughuli zao za kilimo cha Kahawa.

Amesema gharama za matibabu bila kutumia bima ya afya zipo juu na kuwataka viongozi hao wa ushirika kuwahamasisha wanachama wao kujiunga kwa wingi ili kuanza kunufaika na mpango wa serikali wa mazao matano ya kimkakati unaleta matokeo yaliyokusudiwa.

Meneja wa Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) mkoa wa Arusha,Isaya Shekifu akizungumza wakati wa mkutano na viongozi wa vyama vya msingi vya Ushirika wa mazaoa na mfuko huo,kushoto ni Afisa Matekelezo wa NHIF,Miraji Kisile na Mrajisi wa Ushirika mkoa wa Arusha,Emmanuel Sanka.
Baadhi ya viongozi wa vyama vya msingi vya Ushirika wa mazao mkoa wa Arusha wakiwa kwenye mkutano ulioandaliwa na Mfuko wa Bima ya Afya(NHIF) kwaajili ya kuwapa uelewa wa namna ya kujiunga jana,Emmanuel Sanka.Picha na Filbert Rweyemamu 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...