BENKI ya NMB imetoa msaada wa kompyuta tano kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla fupi ya kukabidhi kompyuta hizo, Dar es Salaam leo, Meneja wa NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd alisema kompyuta hizo zitachangia kuongeza ufanisi katika ufundishaji na ujifunzaji hasa kipindi hiki ambacho dunia inaongea zaidi juu ya sayansi na teknolojia.

"Kompyuta tunazozitoa leo hii ni sehemu ya mchango wetu kwa jamii tunaimani zitaweza kuleta matokeo chanya kwa wanafunzi hususani kwenye masomo ya Tehama" alisema Idd.Aliongeza kuwa kompyuta hizo tano zitasaidia kuimarisha mafunzo ya Tehama shuleni hapo na kuongeza uelewa mzuri wa masomo ya Tehama kwa wanafunzi wawapo shuleni na hata baada ya kumaliza masomo yao.

Idd alisema kuwa kompyuta hizo ni sehemu ya kompyuta 150 zinazopelekwa mashuleni kwa mwaka huu ambapo pia katika Wilaya ya Same wamebahatika kupata mgao wa kompyuta tano.

Akizungumzia kuhusu benki hiyo alisema ndiyo inayoongoza nchini kwa kuwa na matawi mengi kwani ina matawi zaidi 228, ATM zaidi ya 800 nchi nzima, NMB wakala zaidi ya 6000 pamoja na idadi ya wateja zaidi ya milioni 3 idadi ambayo ni hazina kuwa ukilinganisha na benki zingine na kuwa imezifikia wilaya zote kwa asimilimia 100 pamoja na kuboresha huduma za kibenki kwa njia ya mtandao ili kufikisha huduma za kibenki kwa wananchi wengi.
Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akimkabidhi, Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, moja kati ya kompyuta tano zilizotolewa na benki hiyo leo hii kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wa shule hiyo. Wa pili  kutoka kushoto ni Meneja wa benki hiyo, Tawi la Msasani, Halima Mcharazo. Wengine ni wanafunzi wa shule hiyo.
 Meneja wa benki hiyo, Tawi la Msasani, Halima Mcharazo, akizungumza kwenye hafla hiyo.
 Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Mikocheni, Salama Ndyetabura, akizunguza wakati akipokea msaada huo.
 Meneja wa Benki ya NMB Kanda ya Dar es Salaam, Badru Idd, akizungumza kwenye hafla hiyo.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...