NAIBU wa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mh. Josephat Kandege leo amefungua kongamano la 10 kwa wadau wa elimu kujadili ufundishaji wa umahiri na ujuzi kwa wanafunzi ili uwasaidie kukabiliana na changamoto zinazowakabili kwa sasa.

Kongamano hilo lililoratibiwa na Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT) limefunguliwa leo Jijini Dodoma na Mh. Kandege kwa niaba ya waziri wake huku akiwapongeza wadau hao kwa juhudi za kuendelea kuiboresha elimu, hivyo kuwahakikishia Serikali inasubiri kwa hamu mapendekezo ya kongamano ili iyafanyie kazi.

Alisema hapo nyuma ilifika kipindi vijana walikuwa wakifundishwa namna ya kujibu mitihani jambo ambalo limekuwa changamoto kijana huyo anapoingia mtaani na kukuta mambo tofauti. "Tunasema tunataka kufanya mapinduzi lazima hivyo lazima twende pamoja kama hivi na kuibuka na majibu," alisema.

"...Haya ambayo mnaenda kuyafanya kwa siku mbili hizi mnazokutana tunaamini kazi nzuri ambayo unaenda kuifanya inakwenda kuliokoa taifa la Tanzania kutoka katika hali ambayo watu wengi wamekuwa wakitilia mashaka juu ya elimu yetu...na sasa tunakwenda kuwa taifa litakalopigiwa mfano kwa ubora wa elimu."
Naibu wa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI), Mh. Josephat Kandege ambaye pia ni mgeni rasmi akizungumza kwenye kongamano la 10 kwa wadau wa elimu kujadili ufundishaji wa umahiri na ujuzi lililoandaliwa na TenMeT. Kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Dodoma, Tumsifu Mwasamale akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dodoma kwenye kongamano hilo. 
Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao (wa pili kulia) akizungumza kwenye kongamano la 10 kwa wadau wa elimu kujadili ufundishaji wa umahiri na ujuzi lililoandaliwa na TenMeT. Kutoka kushoto ni Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Dodoma, Tumsifu Mwasamale akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dodoma kwenye kongamano hilo na Naibu wa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Josephat Kandege, pamoja na Mkurugenzi wa Right To Play Tanzania, Josephine Mukakausa. 
Afisa Maendeleo ya Vijana Mkoa wa Dodoma, Tumsifu Mwasamale (katikati) akimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dodoma akizungumza kwenye kongamano la 10 kwa wadau wa elimu kujadili ufundishaji wa umahiri na ujuzi lililoandaliwa na TenMeT. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mafunzo ya Ualimu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mwl. Augusta Lupokela na kulia ni mgeni rasmi. 
Mkurugenzi wa Right To Play Tanzania, Josephine Mukakausa (kulia) akizungumza kwenye kongamano hilo. Kutoka kushoto ni Naibu wa Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mh. Josephat Kandege, na Mratibu wa Mtandao wa Elimu Tanzania (TenMeT), Bi. Cathleen Sekwao. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...