Ni baada ya kupatikana na hatia ya kukutwa na dawa za kulevya kilogramu 3.03
Na Karama Kenyunko, Blogu ya jamii
MAHAKAMA Kuu Kitengo cha Uhujumu Uchumi jijini Dar es Salaam, imemuhukumu Mwanamke mmoja wa Msumbiji Ana Moisie Chissano kifungo cha maisha baada ya kupatikana na hatia katika shtaka la kukutwa na kilogramu 3.03 za dawa za kulevya aina ya cocaine Hydrochloride.
Mshtakiwa amefungwa chini ya kifungu cha sheria cha 15(1)(b) cha sheria namba 5 ya 2015 cha sheria Kuzuia na kusababisha na kupambana na dawa za kulevya.
Hukumu hiyo imesomwa leo Desemba 12, 2018 na Jaji Lilian Mashaka baada upande wa mashtaka kuweza kuthibitisha mashtaka hayo pasipo Kuacha shaka baada ya kuridhika na ushahidi wa mashahidi sita wa upande wa mashtaka waliofika mahakamani hapo kutoa ushahidi wao.
Aidha Mahakama imeamuru dawa hizo za kulevya kuteketezwa kwa utaratibu unaostahili.

Mshtakiwa Ana
Moisie Chissano raia wa Msumbiji aliyehukumiwa kifungo cha maisha
baada ya kupatikana na hatia katika shtaka la kukutwa na Kg 3.03 za
dawa za kulevya aina ya cocaine Hydrochloride.
Pichani kati ni Mshtakiwa akiwa katika ukumbi wa wazi wa Mahakama Kuu Kitengo cha mafisadi akisubiri kusomewa hukumu yake
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...