Na Tiganya Vincent
WANACHAMA wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoani Tabora wametakiwa kutohofia kuwapokea wanachama kutoka Vyama vya upinzani bali wanatakiwa kushirikiana nao katika kukijenga chama hicho ili kiendelee kuwa imara. Kauli hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi wakati wa kumpokea aliyewahi kugombea Ubunge wa Jimbo la Tabora Mjini kwa tiketi ya UKAWA kupitia Chama cha Wananchi (CUF)Peter Mkufya.

Alisema hawana haja ya kuwa na wasiwasi ya kuwapokea wanachama kutoka upinzani wanajiunga na CCM kwa hofu kuwa watachukua nafasi zao au wana nia ya kugombea nafasi mbalimbali za uongozi wa tiketi kupitia CCM. Wakasuvi alisema jambo la msingi ni CCM kuwa na wanachama imara ambao watakaosaidia kukijenga Chama hicho na kukifanya kiendelee kuwa imara zaidi .

Aidha Wakasuvi alimtaka mwanachama huyo mpya wa CCM Mkufya kutumia muda wake wa uanachama kuungana na wenzake wa CCM kujifunza na kutoa maoni na mawazo ambayo yatasaidia kukifanya kuwa imara zaidi. Kwa upande wake Mkufya alisema amelazimika kuachana na Chama cha Wananchi (CUF) na kujiunga na CCM kwa lengo la kuungana na dhamira ya dhati ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika ujenzi wa Tanzania mpya yenye uchumi miara.

Alisema mambo yanayotekezwa na Rais na Serikali yake ndiyo aliyokuwa akiyapigania wakati akiwa upinzani na baada ya kuona Rais anayatekeleza ameona ni vema ahamie sehemu ambayo atasaidia kuyatekeleza na kuwaletea Watanzania maisha bora.
 Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Tabora Hassan Wakasuvi (mwenye kanzu) akipokea kadi kutoka kwa aliyewahi kugombea Ubunge wa Jimbo la Tabora Mjini Peter Mkufya baada ya kukihama Chama cha Wananchi (CUF) na kujiunga na CCM.
Aliyewahi kugombea Ubunge wa Jimbo la Tabora Mjini kwa titeki ya Chama cha Wananchi (CUF) Peter Mkufya(mwenye kofia)  akizungumza baada ya kukihama cha Wananchi (CUF) na kujiunga na Chama cha Mapinduzi (CCM).
Picha na Tiganya Vincent

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...