Na Agness Francis, Blogu ya Jamii

KAMPUNI ya Good Job Entertainments imesema imeona umuhimu wa kutoa fursa kwa Watanzania kuwa na mazoea ya kutembelea utalii wa ndani zikiwamo mbuga za wanyama.

Hivyo kampuni hiyo imeamua kuandaa safari ya kwenda Hifadhi ya Taifa ya Tarangire mkoani Manyara katika msimu huu Sikukuu ya Krismass ambapo Mratibu wa Safari ya keenda Hifadhi ya Taifa ya Tarangire Juma Mtetwa amesema leo jijini Dar es Salaam kuwa safari hiyo itaanza Desemba 24 na kurudi Desemba 26 mwaka huu.

Amefafanua lengo la kuandaa safari hiyo ni kuhamasisha na kuuza elimu ya maisha ya wanyamapori na kupata muda wa kumpumzika katika msimu huu wa Sikukuu ya X-Mas huku akisisitiza uamuzi huo pia unalenga kuunga mkono kauli mbili ya kuhamasisha utalii wa ndani vitendo.

"Washiriki wa safari hiyo wanatakiwa kufanya maombi ya ununuzi wa tiketi mapema Good job Entertainment ambapo Bibi na Bwana itakuwa Sh.350,000 na kwa mtu mmoja ni Sh.200,000,"amesema.Kwa upande wake Ofisa Masoko wa Tarangire National Park Gedfrey Mbona amesema kuwa 

Watanzania watumie fursa ya kuhamasika kutembelea utalii wa ndani ambao baada ya hapo watakuwa mabalozi wazuri wa kuelezea utalii wetu kwa wageni wanaotoka nchi mbalimbali kuja nchini."Tarangire ni nyumbani kwa tembo kwani kuna idadi kubwa ya wanyama hao kuliko mbuga zote hapa nchini.Pia kwenye hifadhi zetu tunao Simba, Duma, Chui, Twiga na wengine wanyama wengine wengi.Tumeajindaa vizuri kuwapokea watalii wetu na tunaimani mtakaporudi majumbani mtakuwa wajumbe wazuri kwa wengine,"amesema.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...