Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania TCRA leo imeendelea na kampeni yake ya Mnada kwa Mnada karibu tukuhudumie mkoani Kigoma ambayo elimu ya watumiaji huduma pamoja na huduma ya utatuzi wa matatizo yatokanayo ya matumizi ya huduma za mawasiliano zinatolewa.

 Akizungumzia kampeni hiyo inayofanyika katika mnada uliopo Mwanga sokoni Manispaa ya Kigoma Ujiji meneja wa TCRA kanda ya kati Bw. Antonio Manyanda amesema kampeni hii inayohusisha TCRA, Jeshi la polisi kitengo cha makosa ya mtandaoni, watoa huduma wa Airtel, Halotel, Tigo, TTCL vodacom, startimes, Ting, Continental na Digitek inalenga katika  kusogeza huduma kwa wananchi wa kawaida na kujipanga na watoa huduma jinsi bora zaidi ya kutatua matatizo ya watumiaji wa huduma za mawasiliano.

Bw. Manyanda amesema wananchi watatatuliwa matatizo yao yote bila gharama zozote na unataka wakazi wa Kigoma na maeneo mengine kujitokeza kwa wingi wanaposikia kampeni imefika katika mikoa yao.

TCRA ikishirikiana na wadau  wake inaendesha Kampeni ya Mnada kwa Mnada Karibu Tukuhudumie   ambayo itazunguka katika mikoa yote 31. Baada ya Kigoma mnada utahamia Mtwara Desemba 14, 2018
Katika Mnada huo wananchi wa Kigoma wamejitokeza kwa wingi katika kuweza kuhudumiwa wadau mbalimbali wa mawasiliano.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...