Karama Kenyunko,Globu ya jamii

MAHAKAMA ya Hakimu Mkazi Kisutu imeamuru madini yenye thamani ya Sh. bilioni 2.5 yataifishwe na kuwa mali ya serikali kwasababu ukwepaji wa kodi ya mrabaha unasababisha Taifa likose mapato.

Pia Mahakama imeamuru wafanyabiashara watatu wa madini wakiwemo raia wawili wa China na mmoja wa India kulipa faini ya Sh.milioni moja kila mmoja au kutumikia kifungo cha miezi miwili kila mmoja.

Wafanyabiashara hao ni Chang Xu, Kai Jiang, Ashok Lavingia na Kampuni ya Sino Africa Collection Ltd waliokuwa wakikabiliwa na mashitaka matano likiwemo la kuwasilisha taarifa za uongo kwa Kamishna wa Madini kwa lengo la kukwepa malipo sahihi ya mirahaba.

Akitoa hukumu hiyo jana , Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi amesema washitakiwa wanatiwa hatiani kwa kukiri kosa na katika kila kosa kila mshitakiwa atatakiwa kulipa Sh. 200,000 na kifungo cha miezi miwili ambapo jumla ni Sh.milioni nne na kifungo cha miezi miwili.Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo, Wakili wa Serikali, Jacqueline Nyantori aliiomba Mahakama kutaifisha madini hayo chini ya Sheria ya Madini inayosomwa sambamba na sheria ya Uwazi na Uwajibikaji ya mwaka 2015.

Hata hivyo, Wakili wa Serikali Wankyo Simon, alidai washitakiwa hao ni wakosaji wa kwanza na makosa yao yanagusa masuala ya rasilimali za nchi.Alidai kesi hiyo inalenga ukwepaji kodi ambayo ndio uchumi wa nchi na unategemewa katika vitu vyote vinavyofanyika kwa wananchi wa Tanzania, hivyo wanaomba adhabu kali itolewe kwa washitakiwa kulingana na sheria zilizopo kwa lengo la kutunza rasilimali za madini.

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...