Maonyesho ya chakula, kahawa na chocolate yamefanyika mjini Riyadh, Saudi Arabia. Ubalozi wa Tanzania nchini Saudi Arabia ulishiriki kwa kuwaalika baadhi ya wafanyabiashara kutoka Tanzania na wafanyabiashara raia wa Tanzania wanaoishi Saudi Arabia.

Katika maonyesho hayo bidhaa za kahawa ya kijani (green beans) zilionyeshwa na kuvutia wanunuzi wengi wa Saudi Arabia ambao waliweka miadi ‘order’ za kuagiza. Bidhaa zingine zilizowekewa miadi ya kuagizwa ni pamoja na korosho, chai, karafuu, hiliki na viungo. Pia watu walitembelea banda la Tanzania walipata fursa ya kuuliza maswali na kupokea taarifa kuhusu uagizaji wa bidhaa na mazao ya kilimo kutoka Tanzania. 

Kampuni mbili za Saudi Arabia ambazo zilipata taarifa za kahawa kutoka Tanzania katika maonyesho yaliyotangulia ya mwaka 2016 na 2017 zilishiriki na kuuza kahawa iliyokaangwa (roasted) kutoka Tanzania kwa wingi. Kampuni hizo ni Roasting House ambayo kahawa yao huipata kutoka Ruvuma, kampuni nyingine ya pili ni Filter Coffee Roasters ambayo kahawa yao huipata kutoka Songwe. Watu wengi walifurika katika mabanda ya makampuni hayo mawili ya Saudi Arabia kununua kahawa ya kutoka Tanzania kwa kuwa ina ubora wa hali ya juu ukilinganisha na kahawa za kutoka maeneo mengine ambayo zilikuwa ikiuzwa. 
 Watu mbalimbali wakipata maelezo ya bidhaa za Tanzania katika banda la Tanzania katika maonyesho ya chakula, kahawa, chai na chocolate mjini Riyadh, Saudi Arabia.
 Wateja wakiwa wamefurika katika banda la kampuni ya Saudi Arabia iitwayo Roasting House ambayo inauza kahawa iliyoakaangwa kutoka mkoa wa Ruvuma nchini Tanzania.
 Watu waliotembelea banda la Tanzania mjini Riyadh wakionja chai na kahawa ya Tanzania ikiwa ni pamoja na kupata vipeperushi vinavyolelezea kuhusu mazao ya Tanzania.
Mmoja ya wafanyabiashara mwanamama kutoka Tanzania akipanga bidhaa zake za asali kahawa na chai katika banda la Tanzania mjini Riyadh, Saudi Arabia.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...