Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha ameitaka Serikali ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara kuhakikisha inahusisha Mamlaka ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA katika ujenzi wa Chuo cha VETA Simanjiro ili miundombinu ya chuo hicho iweze kujengwa kwa utaratibu na viwango vinavyohitajika.

Naibu Waziri Ole Nasha ametoa agizo hilo Mkoani Manyara wakati akikagua eneo ambalo Serikali ya Wilaya hiyo inategemea kujenga Chuo cha Veta kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Hiari ECLAT.

Alisema ni vizuri Mamlaka husika zikahusishwa katika ujenzi wa Chuo hicho tangu hatua za awali na kumtaka Mkurugenzi wa VETA kanda na yule wa Mkoa kufika katika eneo la Emboreet ambako mradi utajengwa kwa lengo la kuongea na wananchi pamoja na wafadhili wa mradi huo ili wazo ambalo limeanza liweze kutekelezwa kwa utaratibu unaostahili.

“Ninyi Halmashauri mnataka kujenga chuo cha Ufundi ni wazo zuri lakini ni lazima kijengwe kwa utaratibu sio kiholela kwa sababu vilianza kuibuka vyuo ambavyo mtu anakuwa na jengo moja anasajili kinaitwa chuo, kuna viwango na masharti ambayo ni lazima yatimizwe kabla chuo kuruhusiwa kufanya kazi, fuateni taratibu hizo ili muweze kuanzisha chuo cha Ufundi,” aliongeza Naibu Wazizri Ole Nasha.







Naibu Waziri Wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Yefred Myenzi kuhusu namna walivyojipanga kujenga Chuo cha Ufundi na Mafunzo ya Ufundi Stadi cha Wilaya katika eneo la Mradi la Emboreet lililoko katika Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akitoa zawadi kwa mmoja wa wanafunzi wa shule ya msingi Kitwai A aliyefanya vizuri katika mitihani ya kuhitimu darasa la saba mwaka 2018. Shule ya Msingi Kitwai A imefaulisha wanafunzi 25 kati ya 28 waliofanya mtihani mwaka huu. 
Naibu Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia William Ole Nasha akiongea na wakazi wa Kata ya Kitwai A iliyoko katika Halmashauri ya wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara ambapo amewataka kuhakikisha wanaandikisha shule wanafunzi wote wenye umri wa kuanza shule bila kuwaacha nyumbani na kuwapangia majukumu mengine. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...