Na Emmanuel Masaka,Globu ya jamiii

NAIBU Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Abdalah Ulega amempa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara mwezi mmoja wa kuandaa miundombinu ya wafugaji wa vijiji,Vilima Vitatu,Minjingu waliohamishwa katika hifadhi ya wanyamapori ya Burunge.

Ulega amesema Mkurugenzi huyo Hamis Malinga anapaswa kuandaa miundombinu hiyo ya wafugaji ili wakiondolewa kwenye hifadhi ya jamii ya Burunge waweze kuhamia Mfulang'ombe kwenye eneo lililojengwa.

Amesema wafugaji hao wanapaswa kuwekewa miundombinu rafiki ikiwemo malambo na majosho ili waweze kuanza maisha mapya ya ufugaji. Amesema wafugaji hao walikuwa wanalalamikia kuondolewa kwenye eneo hilo na kupelekwa sehemu nyingine ambayo haina miundombinu rafiki.

Hata hivyo, Mkurugenzi Mtendaji wa halmashauri ya Wilaya ya Babati, Hamis Malinga amemuhakikishia Naibu Waziri kuwa wapo kwenye mchakato wa kuandaa miundombinu rafiki ya wafugaji hao. "Kila mfugaji atapatiwa ekari tatu kwa ajili ya kuhakikisha anazimiliki na tutaandaa malambo na majosho kwa ajili ya mifugo ya hizo kaya 17 zilizoondolewa kwenye hifadhi," amesema.

Kwa muda mrefu kaya 17 za wafugaji wa jamii ya kifugaji ya wabarbaig waliamriwa kuondoka kwenye eneo hilo lakini waligoma.

Eneo la jamii la hifadhi ya wanyamapori Burunge lenye ukubwa wa kilomita za mraba 283 linaundwa na vijiji 10 vya Sangaiwe, Mwada, Ngoley, Vilima Vitatu, Minjingu, Kakoi, Olasiti, Manyara, Magara na Maweni. 

Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa kijiji cha Minjingu na Vilima Vitatu wilaya ya Babati mkoani Manyara ,katika mkutano wa hadhara wa kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji,wavuvi na kuzitafutia ufumbuzi .
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwa na kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Babati mkoa Manyara wakiangalia hifadhi ya jamii ya Burunge.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akiwasikiliza wafugaji wa wilaya ya Babati mkoa Manyara walipokuwa wakiwasilisha changamoto zao.
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Abdallah Ulega akizungumza na watumishi wa mkoa wa Manyara katika ziara yake ya kusikiliza kero mbalimbali za wafugaji na wavuvi na kuzitafutia ufumbusi.(Picha na Emmanuel Massaka,MMG)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...