Waziri
Mkuu Mstaafu na Katibu Mkuu Mstaafu wa Umoja wa Nchi Huru za Afrika
(OAU) Dr Salim Ahmed Salim leo asubuhi ametembelea ubalozi wa taifa la
Marekani kutoa salamu za rambirambi kwa serikali na watu wa Marekani
kutokana na msiba wa Rais wa 41 wa taifa hilo Bwana George W. H Bush.
Mheshimiwa
Salim ni mmoja wa watanzania wachache waliopata nafasi ya kufanya kazi
na kumjua Marehemu Bush Snr wakati Mheshimiwa Salim alipokuwa Mwakilishi
wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa na Rais Bush Snr akiwa
Mwakilishi wa Kudumu wa Taifa la Marekani .
Moja ya mambo yaliyowakutanisha ni pamoja na harakati na hatimaye tukio la Taifa la China kurejeshewa haki na hadhi yake ya Uanachama wa Umoja wa Mataifa mnamo mwaka 1971.
Pichani Mheshimiwa Salim akipokewa na Kaimu Balozi wa Marekani Bwana Andy Karas na Naibu Kaimu Balozi Bwana Brian Rettmann.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...