Na Karama Kenyunko, globu ya jamii

MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Freeman Mbowe anayekabiliwa na kesi ya jinai namba 112 ya mwaka huu na wenzake nane, leo Januari 17,2019 ameshindwa kufika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuhudhuria kesi hiyo kwa kuwa anaumwa.

Wakili wa Serikali, Patrick Mwita ameeleza hayo, mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu wa Mahakama hiyo, Wilbard Mashauri wakati kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya washtakiwa kusomewa maelezo ya awali (PH). 

Wakili Mwita amedai kesi hiyo leo,ilikuja kwa ajili ya kutajwa lakini wamepata taarifa kutoka Magereza kuwa mtuhumiwa ameshindwa kufika mahakamani kwa sababu anaumwa hivyo, ameiomba mahakama kuipangia tarehe nyingine kutokana na usikilizwaji wa rufaa ya dhamana ya washatakiwa Mbowe na Mbunge wa Tarime Mjini Ester Matiko kwenye Mahakama ya Rufaa.

Baada ya kusikiliza hoja hizo, Hakimu Mashauri ameahirisha kesi hiyo mpaka Januari 31 mwaka huu.Mbali na Mbowe na Matiko, washtakiwa wengine wanaokabiliwa na kesi hiyo ni Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar Salum Mwalimu na Naibu Katibu Mkuu bara John Mnyika ambaye pia ni Mbunge wa Kibamba.

Wengine ni Mbunge wa Tarime Vijijini, John Heche, Mbunge wa Kawe Halima Mdee, Mbunge wa bunda, Esther Bulaya, Katibu Mkuu wa Chama hicho, Dk. Vincent Mashinji na Mbunge wa Iringa Mjini Peter Msigwa.

Washtakiwa hao kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka 13, ikiwemo kula njama, kufanya mkusanyiko wenye ghasia, kuhamasisha hisia za chuki, kushawishi hali ya kutoridhika, uchochezi na kushawishi utendaji wa kosa la jinai kati ya Februari 1 na 16, 2018, Dar es Salaam.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...