Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MKOA wa Dar es Salaam umeweka wazi mipango yake ya kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa madarasa 622 unakamilika kwa wakati lengo la kufanikisha wanafunzi 31,092 ambao ni sawa na asilimia 47 ya watoto 64,861 waliofaulu katika mkoa huo wanaendelea na masomo yao ya kidato cha kwanza.

Lengo kuu ni kuhakikisha hakuna mwanafunzi yoyote ambaye ataachwa kwasababu ya kigezo cha uhaba wa madarasa huku Mkoa huo ukisisitiza umejipanga vema katika hilo kwa kuweka mikapango sahihi yatakayofanikisha lengo hilo.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda amewaambiwa waandishi wa habari leo kwamba wanafunzi hao wote watakwenda shuleni na kwamba ongezeko la wanafunzi na ufaulu ni matokeo ya mafanikio ya Rais Dk.John Magufuli kutokana na kutengwa kwa fedha zaidi ya Sh.bilioni 29 kila mwezi kwa ajili ya kufanikisha elimu bure na kati ya fedha hizo Sh.bilioni 17.46 zinaenda kwenye elimu ya sekondari.

"Tayari Serikali imejipanga na tayari tangu Januari 7 mwaka huu shule zote za sekondari 147 zimefunguliwa, hivyo kila mzazi ahakikishe anamuandikisha mtoto ili kuendelea na kidato cha Kwanza,"amesema na kusisitiza wanafunzi, wazazi na walezi wasiwe na wasiwasi kwenye hilo kwani wanaotakiwa kwenda shule wote watakwenda.

Wakati huo huo Makonda amesisitiza katika matokeo ya mtihani wa darasa la saba kwa Mkoa wa Dar es Salaam umekuwa kinara kutokana na kufaulisha wanafunzi 64,861 sawa na asilimia 92 ambapo kati ya hao wanafunzi 31,092 walikosa vyumba vya madarasa jambo lililoilazimu Serikali kupambana kuhakikisha kila aliefaulu anaendelea na masomo.

Ameongeza lengo la ujenzi wa madarasa hayo ni kuhakikisha kila mwanafunzi anatumia fursa ya elimu bure inayotolewa na Rais Magufuli ya kuhakikisha mtoto wa maskini anasoma ili kujikwamua kiuchumi na mwisho wa siku Taifa liwe na wataalamu wa kutosha.Makonda ametumia nafasi hiyo kutoa onyo kwa wanafunzi ambao watabainika kukwepa masomo kwani watachukuliwa hatua kali kwa mujibu wa kisheria na hivyo wote ambao wamefaulu na wanatakiwa kuingia kidato cha kwanza waendelee na masomo.
 Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh.Paul Makonda akisikiliza kwa makini baadhi ya maswali yaliyokuwa yakiulizwa na baadhi ya Waandishi wa Habari aliyokuwa akizungumza nao leo Ofisini kwake kuhusu mipango yake ya kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa madarasa 622 unakamilika kwa wakati, lengo la kufanikisha wanafunzi 31,092 ambao ni sawa na asilimia 47 ya watoto 64,861 waliofaulu katika mkoa huo wanaendelea na masomo yao ya kidato cha kwanza.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Mh.Paul Makonda akisizungumza mbele ya Waandishi wa Habari leo Ofisini kwake  kuhusu mipango yake ya kuhakikisha ujenzi na ukarabati wa madarasa 622 unakamilika kwa wakati, lengo la kufanikisha wanafunzi 31,092 ambao ni sawa na asilimia 47 ya watoto 64,861 waliofaulu katika mkoa huo wanaendelea na masomo yao ya kidato cha kwanza.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...