Jamii ya wafugaji imetakiwa kuhakikisha watoto wao wanajiunga na shule za msingi na sekondari, mara baada ya shule hizo kufunguliwa wiki hii na kuachana na mtindo wa kuhamahama na mifugo. Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Sipitieck ameyasema hayo wakati akimsimika Diwani wa Kata ya Naisinyai Kilempu Ole Kinoka kuwa kiongozi wa kimila (Laigwanani) wa Jumuiya ya Kishapuy. 

Sipitieck alisema jamii ya wafugaji inatakiwa kubaki eneo moja kusomesha watoto wao na kuachana na maisha ya kuhamahama na watoto wao ili kutafuta malisho ya mifugo. "Hivi sasa serikali imewekeza miundombinu bora kwenye elimu hivyo jamii ya wafugaji inapaswa kutumia fursa hiyo kwa kusomesha watoto," alisema. 

Hata hivyo, alisema wilaya hiyo imejipanga kuhakikisha wanafunzi wapya wa shule za msingi na sekondari wanapata nafasi kwa kuongeza vyumba vya madarasa. Ole Kinoka akizungumza baada ya kusimikwa ameomba ushirikiano kwa viongozi na jamii kwa ujumla ili aweze kutumikia vyema nafasi hiyo.
 Diwani wa Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Kilempu Ole Kinoka akizungumza baada ya kusimikwa kuwa kiongozi mkuu wa kimila (Laigwanani) wa jamii ya Kishapuy. 
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Sipitieck (kulia) wakishuhudia ngoma ya jamii ya wamasai wakati wa kusimikwa kwa Diwani wa Kata ya Naisinyai Kilempu Ole Kinoka (wapili kulia) kuwa kiongozi wa kimila (Laigwanani) wa jamii ya Kishapuy. 
 Diwani wa Kata ya Naisinyai Wilayani Simanjiro Mkoani Manyara, Kilempu Ole Kinoka akikabidhiwa katiba ya jamii ya Kishapuy na Mwenyekiti wa Halmashauri hiyo, Jackson Sipitieck baada ya kusimikwa kuwa kiongozi wa kimila (Laigwanani) wa jamii hiyo. 
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Simanjiro Mkoani Manyara, Jackson Leskary Sipitieck akizungumza baada ya kumsimika Diwani wa Kata ya Naisinyai, Kilempu Ole Kinoka kuwa kiongozi wa kimila (Laigwanani) wa jamii ya Kishapuy. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...