Na Ofisa Habari Mufindi 

Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi imetiliana saini na Mafundi Uashi saba (07), watakaotekeleza kandarasi za awamu ya kwanza ya ujenzi wa Hospitali ya kisasa ya Wilaya katika kata ya Igowole, eneo ambalo liliteuliwa rasmi kuwa makao makuu mapya ya Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi.

Hafla fupi ya kusaini kandarasi hizo imefanyika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, ambapo, jumla ya Majengo saba muhimu yatajengwa ambayo ni Jengo la Utawala, Jengo la Wagonjwa wa nje, Jengo la kuhifadhia dawa, Jengo la kufulia, Jengo la Mionzi, Jengo la Wazazi sanjari na Jengo la Maabara ambayo yanatajikiwa kukamilika ndani ya kipindi cha miezi nane (08)

Aidha, kiasi cha Fedha kitakachotumika kutekeleza awamu ya kwanza ya mradi huu mkubwa na muhimu kwa ustawi wa Afya za wakazi wa Mufindi ni shilingi Milioni elfumoja na miatano (1,500) sawa na shilingi Bilioni 01 na Milioni 500 zilizotolewa na Ofisi ya Rais – TAMISEMI.

Akizungumza katika hafla ya kutiliana saini, Mwenyekiti wa Halmashari Mhe. Festo Mgina, amewataka Mafundi hao kutekeleza maradi kwa wakati sanjari na kuzingatia viwango vilivyokubalika na atahakikisha wanapata vifaa na malipo yao kwa wakati ili Hospitali hiyo ikamilike kwa wakati na kuanza kutoa huduma kwa wakazi wa Halmashauri ya Mufindi.

Naye kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri Bw. Isaya Mbenje, ametoa rai kwa wataalamu hao wa ujenzi kufanya kazi kwa weledi mkubwa, kuacha visingizio vya mara kwa mara vitakavyochelewesha kukamilika kwa mradi.

“Pigeni kazi Fedha tunayo, yote ipo kwenye akaunti inawasubiri ninyi, hivyo yeyote atakayekwamisha tutavunja mkataba, atafukuzwa pamoja na kufunguliwa mashitaka” akihitimisha Ofisa Mtendaji Mkuu huyo.

Imetolewa na
Ofisa Habari, Mawasiliano na Uhusiano
HALMSHAURI YA WILAYA MUFINDI
  ikionesha ramani ya majengo mara baada ya kukamilika
Mafundi wateule wakisaini kandarasi za ujenzi wa Hospitali ya Wilaya.
 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mhe. Festo Mgina kushoto, akikabidhi mkataba kwa mmoja kati ya Mafundi Saba walioshinda zabuni ya kujenga Hospitali.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...