Angela Msimbira OR-TAMISEMI.

Halmashauri nne (4) zimetuhumiwa kwa ubadhilifu wa zaidi ya shilingi milioni 785 fedha zilizotolewa kupitia mradi wa Equip-T kwa ajili ya kutekeleza kazi mbalimbali za Elimu katika halmashauri hizo. 

Hayo yamesemwa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo alipokuwa akiongea na waandishi wa habari juu ya tuhuma za ubadhilifu katika kikao kilichofanyika Makao Makuu ya TAMISEMI, Jijini Dodoma 

Amezitaja Halmashauri ambazo zimetumia fedha hizo kinyume na utaratibu kuwa Manispaa ya Kigoma, Butiama, Liwale na Bahi ambapo hadi kufikia sasa halmashauri hizo hazijaweza kurejesha fedha hizo TAMISEMI tangu agizo lilipotolewa. 

Mhe. Jafo amesema OR-TAMISEMI iliziagiza Halmashauri 8 ambazo zilituhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha hizo kuzirejesha lakini mpaka sasa ni Halmashauri nane tu ndizo zilizorejesha fedha hizo kwa wakati na hizo zilizobakia kuonyesha utovu wa nidhamu kwa kutotii maagizo ya Serikali. 

“Inasikitisha kuona baadhi ya Halmashauri kushindwa kutii maagizo yanayolewa na Serikali ya kutaka Halmashauri zilizotuhumiwa kwa ubadhilifu wa fedha za Equipt T kurejesha fedha hizo ili ziweze kutekeleza miradi ya elimu nchini” anasema. 

Ameendelea kufafanua kuwa amesikitishwa zaidi na Manispaa ya Kigoma Ujiji na Butiama kutokana na kuwa na tuhuma nyingi za ubadhilifu wa fedha za miradi mbalimbali inayotekelezwa katika Halmashauri hiyo. 

Mhe. Jafo ameziagiza Halmashauri ambazo bado hazijakamilisha kurejesha fedha hizo kuhakikisha zinawasilishwa kabla ya tarahe 28/3/2019. 

Amezielekeza mamlaka husika kuwachukulia hatua za kinidhamu na kuwashusha vyeo Afisa Mipango, Mweka Hazina na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Butiama kwa kushindwa kutimiza wajibu wao. 

Mhe. Jafo ameitaka mamlaka inayohusika kufanya uchunguzi wa aliyekuwa Mkurugenzi, amemuagiza Katibu MMkuu OR-TAMISEMI kuwachukulia hatua Mweka Hazina wa Halmashauri ya Bahi Said Ishabairu ambaye alihamishiwa katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa. 

“Kumekuwa na tabia kwa baadhi ya watumishi kuhamishwa maeneo ya kazi pale wanapokosea, hili si jambo jema Serikali haitavumilia bali itawachukulia hatua za kinidhamu watumishi wote wanaoihujumu Serikali popote pale watakapokuwa” alisema. 

Aidha ameziagiza Mamlaka husika kumtafuta aliyekuwa Mweka Hazina wa Manispaa ya Kigoma Ujiji ambaye kwa sasa amestaafu ili aweze kuhojiwa kwa tuhuma hizo. 

Jafo aliongeza kuwa Serikali haitavumilia mambo yeyote ambayo yanaleta hujuma katika suala zima la kuwahudumia watanzania hivyo amewataadharisha Wakurugenzi wote katika Halmashauri za Mamlaka za Serikali za Mitaa kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa katika matumizi ya fedha za miradi mbalimbali ya maendeleo. 

Jafo alimalizia kwa kumuagiza Naibu Waziri Mhe. Mwita Waitara kusimamia kwa makini miradi ya elimu na kuangalia namna fedha zilizvyotumika katika miradi hiyo agizo ambalo Mhe. Mwita amesema alalitekeleza kwa umakini mkubwa. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...