*TANESCO yazungumzia faida zake ikiwamo ya kuiwezesha Tanzania kuuza au kununua umeme kwa nchi nyingine za Afrika
*Wananchi ambao mradi huo unapita washauriwa kutoa ushirikiano ili kuhakikisha kazi inakwenda kama ilivyokusudiwa

Na Said Mwishehe,Globu ya jamii

MRADI mkubwa wa umeme unaotekelezwa na Serikali ya Awamu ya Tano kupitia Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) ambao utaiwezesha nchi kununua au kuuza umeme katika nchini za Afrika umeanza kutekelezwa ambapo kwa sasa mradi wa kuunganisha umeme katika nchi za Kenya na Tanzania umeanza.

Mradi huo unafahamika kwa jina la Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP) ambapo kutakuwa na hatua mbalimbali za kuutekeleza mradi huo uliogawanywa katika hatua nne za utekelezaji wake huku TANESCO ikifafanua umuhimu na faida lukuki za mradi utakapokamilika na kwa sasa wakandarasi wapo kazini na kanzi imeanza kufanyika.

Kwa mujibu wa TANESCO awamu ya kwanza itakuwa ni kuzinganisha nchi za zilizopakana na Tanzania kuwa na umeme wa uhakika huku awamu ya pili ya mradi huo ukihusisha nchi za Tanzania na Zambia (ZTK) ambao nao tayari umeanza kutekelezwa ambapo kazi ya kutengeneza misingi ya kusimika minara imeanza.Akiuzungumzia mradi huo jana jijini Arusha, Mratibu na Msimamizi wa Mradi huo kutoka Shirika la Umeme Tanzania (Tanesco), Mhandisi Peter Kigadye, amefafanua mradi huo wanaamini utakamilika kwa wakati kama ambavyo wamekubaliana na wakandarasi ambao tayari kazini na vifaa vyote muhimu vimefika na kazi ya kusimika nguzo imeanza.

Ameongeza kuwa mradi huo ni sehemu moja ya mradi mzima wa Regional Power Connection ambao lengo lake ni kuunganisha mfumo wa umeme wa Tanzania na Afrika Mashariki (East Africa Power Pool) kwa upande wa Kaskazini na baada ya kukamilika utekelezaji wake itakuwa inaunganisha mifumo ya nchi Kusini mwa Afrika, kupitia mradi wa Southern Africa Power Pool (SAPP).

Amesema kuwa Tanzania imebarikiwa kwai itakuwa na sehemu tatu za mradi huo ambapo ya kwanza ni mradi wa Backborn ambao umejengwa katikati ya nchi yetu na ulikuwa na kilomita 670 inaanzia Shinyanga hadi Iringa wakati sehemu ya pili ni kuunga kutoka Singida hadi mpakani na Kenya ambapo kuna kituo kimoja kinachoitwa Isinya.

"Jumla ya mradi wote una umbali wa kilometa 510 lakini kwa upande wetu Tanzania tunazo kilometa 414 na upande wa Kenya nao wanakilometa 96.Kwa upande wetu tunakwenda vizuri kwani kila kipande cha ujenzi wa mradi kuna mkandarasi wake na kila mmoja yupo hatua mbalimbali za ujenzi.Kupitia watalaam wetu tumekuwa tukifuatilia hatua kwa hatua na wakati huo huo wapo watalaamu wengine ambao nao wanafanya kazi hiyo hiyo kuhakikisha kila kinachofanyika kimezingatia mahitaji na vigezo vya viwango vya ubora,"amesema Mhandisi Kigadye.

Amefafanua pia kutakuwa na sehemu ya tatu ambayo ni Iringa kwenda Kusini ambapo kuna mradi utakaoitwa Zambia Interconector ambako kuna kilomita nyingine 624, hivyo baada ya kukamilika kwa mradi Tanzania itakuwa imekamilisha ule mkongo wa msongo wa Kilovoti 400.Lengo kuu la kuunganisha nchi yetu na ukanda nchi za Kikanda kuanzia Kaskazini kuungana na Kenya na Kusini kuungana na Zambia maana yake ni kuifanya Tanzania kuingia kenye mfumo wa umeme ambao utahusisha nchi mbalimbali za Afrika.

"Tunafahamu mradi huu wa njia ya umeme ya Kenya-Tanzania Power Interconnection (KTIPIP)ZTK, unatarajiwa kukamilika Aprili 2020 na ule Zambia Connector utakamilika mwaka 2022.Hivyo maana yake ni kwamba hii itakuwa tumemaliza mikongo hii mitatu na nchi yetu.Kupitia huu mfumo nchi hizo zitakuwa zimeingia kwenye biashara ya umeme na hakutakuwa na tatizo la umeme tena,"amesisitiza.

Kuhusu mradi wa Kenya-Tanzania Power Interconnection kwa maelezo ya Mhandisi Kigadye amesema sehemu ya kwanza itahusu ujenzi wa njia za kusafirisha umeme na ujenzi wa vituo vya kupozea umeme.

"Kama ambavyo nimeeleza awali jumla ya kilometa za mradi huo ambapo utapita ni 510 na umegawanyika kwenye sehemu nne, ambazo ni Isinya Kenya hadi Namanga Kilomita kilomita 96, sehemu ya pili unahusu Namanga-Arusha Kilomita 114, sehemu ya tatu Arusha-Babati kilomita 150, na Bababti-Singida kilomita 150.Kiasi cha fedha ambacho kitatumika kwa ajili ya mradi huo ni dola za Marekani milioni 258,"amesema Mhandisi.

Wakati huo huo Meneja Mwandamizi wa TANESCO anayehusika na miradi Mhandisi Emmanuel Manirabona amesema katika kuhakikisha mradi huo unakamilika kwa wakati tayari vifaa vyote muhimu tayari vipo maeneo y mradi na wakandarasi wanaendelea na ujenziAmetumia nafasi hiyo kuzungumzia umuhimu wa wananchi ambapo mradi utapita kutoa ushirikiano ili kufanisha mradi na hasa kwa kuzingatia TANESCO imeshalipa fidia kwa watu wote ambao wanastahili na hivyo haitarajii kuona watu wengine wanajitokeza na kukwamisha ujenzi huo kwa kigezo cha kudai fidia.

Mhandisi Manirabona ameelezea matumaini ya TANESCO baada ya kukamilika kwa mradi huo ambao utatoa fursa ya nchi moja kununua umeme kwa nchi nyingine iwapo itahitajika kufanya hivyo lakini kwa Tanzania mradi huo umekuja wakati muafaka hasa kwa kuzingatia nchi inatekeleza ujenzi wa viwanda , na hivyo mwito wao ni kuhamasisha watu kuwekeza kwa kujenga viwanda maeneo mbalimbali nchini kwani hakuna tatizo la nishati ya umeme.
Baadhi ya vifaa ambavyo vipo kwenye eneo la ujenzi wa mradi wa umeme unaoendelea mkoani Arusha.

 Meneja Mwandamizi wa Shirika la Umeme Tanzania(TANESCO) anayehusika na miradi Mhandisi Emmanuel Manirabona akifafanua jambo kuhusu ujenzi wa mradi wa kuunganisha umeme unaendelea mkoani Arusha
 Shughuli za ufungaji vifaa ukiendelea 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...