Na OWM (KVAU) – Tabora

Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu inaratibu mafunzo maalum kwa mama wadogo yanayolenga kuwawezesha kujitambua na kujithamini.

Mafunzo hayo yamefanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Uyui iliyopo Mkoani Tabora ambapo mama wadogo takribani 45 wamefundishwa mada mbalimbali ikiwemo Ujasiriamali, kilimo biashara, taratibu za kuunda vikundi vya uzalishaji mali, fursa za uwezeshaji wa vijana kiuchumi, malezi bora na familia, afya na lishe.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Msuya amesema kuwa Serikali inatambua tatizo la mimba za utotoni na imeonesha dhairi ufuatiliaji wa suala hilo kwa kuwachukulia hatua za kisheria wanaohusika na vitendo hivyo.

“Takribani asilimia 45 ya mabinti wanaoandikishwa kujiunga na kidato cha kwanza wanashindwa kumaliza kidato cha nne kutokana na changamoto za mimba za utotoni, ndoa za utotoni na umbali wa kupata huduma ya elimu.” alisema Msuya .Aidha, Msuya alieleza kuwa Halmashauri yake imeanzisha kampeni ya “Nishike Mkono, Boresha Elimu Uyui” inayolenga kuwainua watoto wa kike kwa kuwaboreshea mazingira ya elimu yatakayo wawezesha kupata elimu bora.


Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Msuya akizungumza na Mama Wadogo (Young Mothers) wakati wa ufunguzi wa mafunzo yaliyofanyika Wilaya ya Uyui, Mkoa wa Tabora. 
Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Vijana Bw. Julius Tweneshe akifafanua jambo kwa Mama wadogo walioshiriki mafunzo hayo kuhusu malengo ya mafunzo hayo yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu). 
Afisa Maendeleo ya Vijana kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Bi. Atupokile Mhalila akitoa mada kuhusu Mfuko wa Maendeleo ya Vijana kwa Mama wadogo walioshiriki kwenye maunzo hayo yalifanyika Wilaya ya Uyui. 


Baadhi ya Mama wadogo wakifuatilia hotuba ya Mkuu wa Wilaya ya Uyui Mhe. Gift Msuya (hayupo pichani) wakati wa ufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika kwenye ukumbi wa Halmashauri ya Uyui. 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...