WANAFUNZI  wote 135 waliofanya mtihani wa kidato cha nne katika shule ya St Anne Marie wamefaulu kuendelea na kidato cha tano wakiwa na ufaulu wa juu.

Kwenye matokeo hayo yaliyotangazwa hivi karibuni na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA), kati ya wanafunzi hao, wanafunzi 28 wamepata daraja la kwanza, wanafunzi 58 daraja la pili na wanafunzi 49 wamepata daraja la tatu.

Akizungumzia matokeo hayo, Mkuu wa shule hiyo, Gladius Ndyetabura alisema hayo ni mafanikio makubwa kwa shule yake kuzingatia idadi kubwa ya wanafunzi waliokuwa nao.Aliwashukuru wazazi wa wanafunzi kuwa wamekuwa chachu ya ushindi huo kutokana na ushirikiano wanaotoa kwa uongozi wa shule hiyo kuanzia shule ya msingi hadi sekondari.

Ndyetabura aliwashukuru pia walimu wa shule hiyo kwa namna wanavyojituma usiku na mchana kuhakikisha wanafunzi wanaofanya mtihani wanapata alama za juu.

“Shukrani za kipekee ziwaendee walimu wangu kwasababu hawapumziki wanafanyakazi usiku na mchana, Mkurugenzi  wa shule Jasson Rweikiza naye amekuwa nguzo kubwa kwenye ushindi huu kwa namna anavyotupa kila aina ya ushirikiano tunampongeza sana,” alisema  

Aidha, alisema matokeo hayo ni mwendelezo wa mafanikio ya shule hiyo kuanzia kwenye mitihani yaa daarasa la nne, darasa la saba na kidato cha pili.Alitoa mfano kuwa kwenye matokeo yaa darasa la nne mwaka 2018, shule yake iliibuka ya kwanza Wilaya ya Ubungo na ilishika nafasi ya pili kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambapo wanafunzi wake wote walifaulu kwa wastani wa alama A.

Ndyetabura alisema pia kwenye matokeo ya kidato cha pili yaliyotangazwa hivi karibuni, kwa mara nyingine tena St Anne Marie iliibuka kidedea kwa wanafunzi wake 10 kupata daraja la kwanza la point saba.Alisema kwenye matokeo hayo, wanafunzi 45 walipata daraja la kwanza, wanafunzi 14 daraja la pili na wanafunzi wawili ndio walipata daraja la tatu.

“Haya ni mafanikio makubwa sana kwetu hata wazazi wametupongeza sana kwa ufaulu huu kwasababu wanafunzi wetu wote wanakwenda kidato cha tano wakiwa na ufaulu wa juu sana tunaomba wazazi waendelee kutuamini na nawaahidi kwamba hatutabweteka ka mafanikio haya,” alisema.

Ndyetabura alisema wanafunzi wote waliofanya vizuri kuanzia darasa la nne, kidato cha pili na wa kidato cha nne walipewa zawadi mbalimbali siku ya Jumamosi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...