NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
SHIRIKA la Umeme Nchini TANESCO limewahimiza wananchi kuwekeza kwenye viwanda kwani hivi sasa umeme bora na wa uhakika upo, Meneja Miradi wa Shirika hilo, anayeshughulikia uzalishaji (Generation) Mhandisi Stephene S. A. Manda (pichani juu) amesema leo Januari 9, 2019.
Amesema hayo jijini Dar es Salaam wakati akielezea utekelezaji wa miradi ya umeme Kinyerezi II wa Megawati 240 na ule wa upanuzi wa Kinyerezi I wa Megawati 185. “Mradi wa Kinyerezi namba II wa Megawati 240 umekamilika, kwa hivyo ombi letu kwa wote ambao wanaweza kuwekeza kwenye viwanda wawekeze kwani umeme wa uhakika na wa kutosha upo.” Alisema na kuongeza.
Licha ya mradi huo wa Kinyerezi II Mradi mwingine ni wa upanuzi wa Kinyerezi I unaozalisha megawati 150 ili ufikie Megawati 335 kwa kuongeza Megawati 185.“Itakapofika Agosti 2019 jumla ya umeme utakaokuwa unatoka Kinyerezi pekee ni Megawati 575 kwa hivyo ni umeme wa kutosha, kama ni kulisha Dar es Salaam, basi Dar es Salaam nzima Kinayerezi inaweza kuibeba.” Alitoa hakikisho.
Kwa hivyo uwezo wa kuhakikisha viwanda vinapata kile vinavyopasa kupata kuhusiana na umeme TANESCO imejipanga vizuri na tunaomba sana wawekezaji wawekeze, kiwanda si lazima kiwe kikubwa sana, hata cha kukoboa na kusaga nafaka na vile vya kukamua matunda ya kutoka Tanga na kwingineko. Alisema Mhandisi Manda. Alitoa wito kwa watanzania kuuunga mkono juhudi za Serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi wake Rais Dkt. John Pombe Magufuli wa kujenga uchumi wa kati na wa viwanda kwani inawezekana kwa vile umeme upo, ulio bora na wa uhakika.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...