Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
Timu
ya Maafisa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto pamoja na Taasisi zake iko katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya
Afya kwa kuangalia uwekezaji katika Sekta ya Afya katika kipindi cha
miaka mitatu ya serikali ya Awamu ya Tano ya Rais Dkt. John Pombe
Magufuli.
Akizungumza
kwenye Kampeni hiyo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili, Mwakilishi wa
Wizara ya Afya na Meneja wa Mawasiliano na Elimu kwa Umma Gaudensia
Simwanza amesema ziara hiyo katika Hospitali na Taasisi zilizo chini ya
Wizara ya Afya ni kuangalia uwekezaji katika utoaji huduma bora za Afya
kwa wananchi,kuhakikisha kuna nguvu kazi imara ya uzalishaji katika
Sekta ya viwanda.
Amesema
kuwa serikali imewekeza sehemu kubwa ya vifaa na mitambo katika
hospitali na hali iliyofanya serikali kuokoa fedha nyingi kutibu
wagonjwa nje ya nchi.
Simwanza
amesema kuwa Hospitali ya MOI imekuwa na vifaa katika kila idara na
kurahisisha utoaji huduma za Afya ambazo ni bora kutokana na Serikali
kutilia mkazo uwekezaji wa vifaa tiba,mitambo, Dawa pamoja na
vitendanishi.
Nae
Afisa Habari wa MOI Patrick Mvungi amesema kuwa MOI itaendelea kutoa
huduma bora kutokana na Serikali kuwekeza mashine mbalimbali zilizo kuwa
changamoto,ambazo zilikuwa zinasababisha wagonjwa kupewa rufaa.
Mvungi
ameipongeza serikali katika uwekezaji uliofanyika Hospitalini hapo
pamoja na ujenzi wa majengo ya kisasa na kulaza wagonjwa kwenye 340
vitanda.Amesema katika ununuzi wa vifaa wamenunua Darubin ya kisasa ya sh.bilioni Moja.
Daktari
Bingwa wa Upasuaji Moyo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI)
Peter Kissenge amesema serikali imenunua mtambo wa sh.Bilioni Tatu na
kufanya Taasisi hiyo kuendelea kutoa huduma bora za Afya ndani na nje ya
nchi.
Kissenge amesema kuwa Taasisi hiyo ni kati ya Taasisi 25 zinazotoa huduma za matibabu ya Moyo katika nchi za Afrika.Amesema magonwa ya Moyo yanatokana na wananchi kushindwa kufanya mazoezi pamoja hali ya ulaji wa vyakula.
Kissenge
amesema kuwa nchi ya Thailand wananchi wake wanatumia baiskeli zaidi
kuliko magari hali hiyo ni tofauti na hapa nchini ambao wanaona kutembea
na magari ni ufahari.
Sehemu
ya kufanyia uangalizi wa magonjwa ya mwili wa binadamu kwa kutumia
mitambo hiyo ambayo imenunuliwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais
Dkt. John Magufuli katika Hospitali ya MOI.
Daktari
wa Hospitali ya MOI Ngina Mitti Akizungumza na waandishi wa habari na
Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia
Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika Kampeni ya
Tumeboresha Sekta ya Afya.
Daktari
Bingwa wa Picha za MRI Rahma Hingora akizungumza na waandishi wa Habari
na Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii,
Jinsia, Wazee na Watoto na Taasisi zilizo chini ya Wizara hiyo katika
Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya katika Hospitali ya Mifupa (MOI)
Jijini Dar es Salaam.
Mgonjwa
wa Figo Magesa Masigi akizungumza namna ya huduma za Afya
zilizoboreshwa katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Jijini Dar es Salaam.
Afisa
Muuguzi mwandamizi wa Kitengo cha Figo Moroa Nyamatara akizungumza na
waandishi wa Habari na Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya
Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto katika Kampeni ya Tumeboresha
Sekta ya Afya jijini Dar es Salaam.
Mratibu
wa Maduka ya MSD Betia Kaema akizungumza na waandishi wa Habari na Timu
ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee
na Watoto katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya.
Duka
la MSD lilopo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambalo limejngwa
katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli.
Afisa
Habari wa MOI Patrick Mvungi akizungumza na waandishi habari kuhusiana
na Mafanikio ya Miaka mitatu ya Rais Dkt John Pombe Magufuli katika
uboreshaji wa upatikanaji wa vifaa katika Hospitali hiyo
Jengo la MOI lilojengwa kwa udhamini wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Daktari
Bingwa wa Hospitali ya MOI Hamis Shaban akizungumza na waandishi wa
Habari na Timu ya Maafisa wa Habari wa Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii
Jinsia Wazee na Watoto katika Kampeni ya Tumeboresha Sekta ya Afya.
Meneja
Uhusiano wa NHIF Akizungumza na wagojwa katika Hospitali ya MOI
kuhusiana na utumiaji wa bima ya Afya katika Hospitali hiyo jijini Dar
es Salaam.
Jengo
la Watoto katika Hospitali ya Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ambapo
limejengwa katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais wa Awamu ya Tano Dkt.
John Pembe Magufuli.
Moja
ya mtambo wa Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete JKCI Ulionunuliwa kwa
sh.bilioni tatu katika kipindi cha miaka mitatu ya Rais Dkt John Pombe
Magufuli.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...