Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii. 
VIGOGO wawili na Wakurugenzi wa Kampuni ya Rifaro Africa Limited, Jones Moshi (42) na James Gathonjia (35),  wamehukumiwa kulipa faini ya zaidi ya Sh. Milioni 200 baada ya kukiri mashtaka ya kuendesha biashara haramu ya upatu na kutakatisha zaidi ya Sh. Bilioni Moja. 

Hukumu hiyo imesomwa leo mchana January 10, 2019 na Hakimu Mkazi Mkuu,  Wilbard Mashauri wa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu baada ya washtakiwa hao kukiri kutenda makosa wao wenyewe. Akisoma hukumu hiyo,  Hakimu Mashauri amesema, mahakama imewatia washtakiwa hao hatiani baada us wao wenyewe kukiri Majira yap. 

"Mahakama imewatia hatiani sababu nyie wenyewe mmekili kutenda makosa", amesema hakimu Mashauri. Akiwasomea adhabu washtakiwa amesema,  Katika kosa la kuendesha biashara haramu ya upatu washtakiwa kila mmoja anahukumiwa kulipa faini ya Sh. Milioni mbili name kama wakishindwa wataenda jela miaka miwili kila mmoja. 

Aidha katika shtaka La kutakatisha Fedha zaidi ya Sh. Bilioni moja kila mshtakiwa anatakiwa kulipa faini ya Sh. Milioni mmoja na Kama akishindwa ataenda jela miaka mitano. Washtakiwa hao ambao wamekaa rumande Kwa takribani mwaka mmoja,  Kwa Kuwa shtaka La kutakatisha fedha lililokuwa linawakabili halina dhamana, wameachiwa huru baada ya kufanikiwa kulipa faini hiyo na kunusurika kwenda jela. 

Kabla ya kusomewa hukumu hiyo, hakimu Mashauri  aliuuliza upande wa mashtaka kama walikuwa na lolote la kusema ambapo wakili wa serikali Mkuu,  Shadrack Kimaro aliiomba mahakama kutoa adhabu inayostahili kwa mujibu wa sheria ili iwe fundisho kwa wengine wanaoweza kufikiri kutenda makosa kama haha. 

Mapema baada ya washtakiwa kukiri kosa walisomewa maelezo ya awali ambapo wanadaiwa kuisajili kampuni hiyo ya Rifaro name kupewa leseni ya kampuni ya kuuza simu  vocha na vifaa vya simu na kwamba waliingia mkataba na kampuni ya simu za mkononi ya Zantel. 

Imedaiwa,  hata hivyo washtakiwa hao walienda kinyume na leseni yao ya biashara na kuanza kuhamaisha watu kujiunga na kampuni hiyo kupitia warsha mbalimbali za vipeperushi kwa kiingilio cha Sh. 76500  ambayo baadae kilipanda na kufikia Sh. 128,000 Huku wanaofanikisha wakipewa muda wa maongezi wa Shule. 5000 name ili mtu apate Faida kubwa alitakiwa kushawishi watu wengi zaidi kujiunga na kampuni hiyo. 

Akisoma Maelezo Hayo,  Kimaro amedai,  fedha zilizopatikana Sh. 1,022, 560, 854 ziliingizwa katika akaunti namba 3301106013 iliyopo Kenya Commercial Bank (T)Ltd (KCB) tawi la Mlimani City yenye jina la Rifaro Africa Limited ambayo  washtakiwa ndio walikuwa Watia saini.

 Katika kesi ilidaiwa, kati ya Julai 14, 2014 na Julai 31, 2016 ndani ya Jiji la Dar es Salaam na maeneo mbalimbali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  waliendesha biashara ya upatu kwa kukusanya fedha kutoka kwa mwananchi kwa ahadi kuwa fedha hizo zitazaa. Pia wanadaiwa kujihusisha na miamala ya fedha moja kwa moja ya Sh. 1,022, 560, 854 kupitia akaunti namba 3301106013 iliyopo Kenya Commercial Bank (T)Ltd (KCB) yenye jina la Rifaro Africa Limited, wakati wakijua fedha hizo ni zao la makosa ya kuendesha biashara ya upatu.

Wakurugenzi wa Kampuni ya Rifaro Africa Limited, Jones Moshi(wa pili kulia) na James Gatuni, wakiingia katika chumba cha Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu Dar es Salaam jana kusikiliza mashitaka ya utakatishaji fedha na Kuendesha mchezo wa upatu katika. PICHA IMANI NATHANIEL

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...