Na Felix Mwagara, MOHA-Biharamulo.
WAZIRI wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola amempa siku 30 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufanya ukaguzi taasisi mbalimbali za umma na binafsi nchini kuwa na vifaa vya zimamoto.
Lugola alisema ukaguzi huo pia ulenge zaidi katika shule za msingi, sekondari na vyuo, vituo vya kutolea huduma za afya ili kuepukana na ajali zitokanavyo na vyanzo vya moto.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na mamia ya wananchi, ambao ulifanyika katika uwanja wa mpira Mjini Biharamulo, Mkoani Kagera, leo, Lugola alisema atafuatilia utekelezaji wa agizo lake kama litakua limefanyiwa kazi jinsi anavyotaka yeye. Pia Waziri Lugola amewaomba Wakurugenzi Watendaji wa Halmashauri zote nchini kuhakikisha wanatenga fedha za mapato ya ndani kununua vifaa za zimamoto katika taasisi za Serikali wanazoziongoza.
“Haiwezekani wanafunzi, wagonjwa katika zahanati mbalimbali au vituo vya afya wapate tatizo la ajali la moto halafu wakurugenzi na mameneja au wakuu wa taasisi hizo wakishindwa kuweka vifaa vya zimamoto licha ya kupokea fedha za kutolea huduma,” alisema Lugola. Aidha, Waziri Lugola amezitaka taasisi za dini kuendesha ibada kwa kuhakikisha majengo yanasajiliwa na pia Miiskiti na Makanisa yasitumike kuhifadhi wahalifu wanaotumia migongo ya kuwa wachungaji na mashekhe kama mwavuli wa maadili mema bila uzalendo.

 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola akizungumza na mamia ya wananchi wa Mji wa Biharamulo, Mkoani Kagera, leo. Lugola amempa siku 30 Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kufanya ukaguzi taasisi mbalimbali za umma na binafsi nchini kuwa na vifaa vya zimamoto.
 Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola (kushoto), akimsikiliza Mkuu wa Jeshi la Magereza Mkoa wa Kagera, Raymond Mwampashe, lipokua anamfafanulia jambo wakati Waziri huyo alipofika katika Gereza la Biharamulo mkoani humo kujua utendaji wa kazi wa Gereza hilo. Katikati ni Mkuu wa Wilaya ya Biharamulo, Saada Malunde.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, akitaka ufafanuzi wa jambo kutoka kwa Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, (RPC) Revocatus Malimi (kushoto), wakati Waziri huyo alipopata malalamiko kuhusu ng’ombe za Mkazi wa Mji wa Biharamulo (kulia) kukamatwa na Polisi Wilayani Biharamulo. Hata hivyo, RPC alimfafanulia Waziri huyo kuhusiana na malalamiko hayo dhidi ya mifugo iliyokamatwa na Polisi na kuhifadhiliwa katika Gereza la Biharamulo. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi. 

KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...